FAIDIKA YAPANUA WIGO WA HDUMA ZAKE,SASA KUHUDUMIA SERIKALINI NA SEKTA BINAFSI ....

TAASISI ya kutoa mikopo ya Faidika
imepewa kibali na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) cha kuwa wakala wa Benki ya
Advance yenye matawi matano nchini yanayotoa huduma za kifedha.Anaandika KAROLI
VINSENT endelea nayo
Kibali hicho kimetolewa baada ya kampuni mama ya Faidika ijulikanayo
kama Letshego Holding Limited ya nchini Botswana, kununua asilimia 75 ya hisa
za Benki ya Advance.
Akizungumza na waandishi wa habari
leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Letshego Group, Chris Low,
alisema hatua hiyo itapanua wigo wa Taasisi ya Faidika katika kutoa mikopo kwa
watu binafsi tofauti na ilivyokuwa awali ambapo ilikua inatoa kwa watumishi wa
umma pekee.
Amesema
utoaji mikopo kwa watu binafsi unatokana na Benki ya Advance kuwa na uzoefu
mkubwa katika kufanya kazi na watu wa aina hiyo hivyo ushirikiano wao
utasaidia kuwafikia watu wengi zaidi.
"Faidika ina vituo 105 kote nchini na hivyo kuwa wakala wa Benki ya
Advance kutasaidia kupanua huduma za benki hiyo ambayo ilikuwa na matawi matano
tu kote nchini yakiwemo matatu jijini Dar es Salaam na mengine mawili mikoani," amesema Low.
Amesema Letshego Group imepiga hatua katika kuhakikisha
kuna mfumo mzuri wa kuwezesha jamii kupata huduma za kifedha kwa urahisi.
“Kufanikiwa kwa benki ya Advance ni
ishara tosha kwa kujitolea kwetu kutoa huduma za kibenki kwa watu wenye kipato
cha chini na cha kati katika jamii yetu, ambao kihistoria hawajaweza kupata
huduma stahiki katika benki za kibiashara,” amesema Low.
No comments
Post a Comment