TAASISI YA DON BOCKO YAWAPA USHAURI BORA WANAWAKE,SOMA HAPO KUJUA
Meneja wa mipango wa kapeni ya Binti Thamani Rosemacy Njoki akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya kampeni ya kuwahamasisha wasichana kupenda kujiunga na vyuo vya ufundi ili kujifunza ufundi stadi na kujiendeleza kimaisha ikiwa ni pamoja na kujipatia ajira endelevu, amesema hayo katika kutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kushotoni Mkuu wa Chuo cha ufundi cha Don Bosco Dodoma Fromac Mulu. |
TAASISI ya kidini ya Don Bosco imeandaa kampeni ya kuwahamasisha wasichana kupenda kujiunga na vyuo vya ufundi ili kujifunza ufundi stadi na kujiendeleza kimaisha ikiwa ni pamoja na kujipatia ajira endelevu.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Meneja wa mipango wa kapeni ya Binti Thamani, Rosemacy Njoki amesema wana vyuo mbalimbali hapa nchini ambavyo vinatoa mafunzo ya ufundi stadi kwa vijana lakini kumekuwa na asilimia ndogo ya vijana wakike wanaojiunga na mafunzo ya ufundi stadi ukilinganisha na idadi ya vijana wa kiume kwa mwaka.
amesema baadhi ya kozi zinazotolewa na vyuo vya Don Bosco vilivyopo Dar es Salaam Dodoma na Iringa ni ufundi Seremala, uchongaji vipuri, uungaji na uundaji vyuma, umeme wa viwandani na majumbani, uhazili, ujenzi, ufundi bomba na magari, ufundi cherehani uchapishaji na kompyuta.
Kampeni ya Binti thamani ni mwendelezo wa uhamasishaji kwa wasichana kuibua na kutatua changamoto mbalimbali za vijana hususani wasichana kutambua kuwa kuna fursa ya kujiendeleza na kufanikiwa kupitia mafunzo ya ufundi baada ya kumaliza mafunzo yao.
Kampeni hiyo itasaidia kuwakumbusha kuwa wasichana nao wana uwezo wa kufanya kazi yoyote hasa anapokuwa na malengo chanya.
Kampeni hiyo leo itawakutanisha
wasichana mbalimbali hasa wanafunzi wa shule za sekondari wapatao 1000 katika
mikoa wa Dar es Salaam.
“Lengo la kampeni hii ni kuwakutanisha wasichana na wadau mbalimbali waliopitia mafunzo ya ufundi stadi na kuwahimiza kuwa mabalozi wazuri katika kuhakikisha wasichana wengi Zaidi wanapenda mafunzo ya ufundi stadi.
“Tunawaomba wazazi na walezi tusaidiane kwa pamoja katika harakati za kuwahamasisha wasichana kwani ndio tegemeo la jamii yetu,
“Lengo la kampeni hii ni kuwakutanisha wasichana na wadau mbalimbali waliopitia mafunzo ya ufundi stadi na kuwahimiza kuwa mabalozi wazuri katika kuhakikisha wasichana wengi Zaidi wanapenda mafunzo ya ufundi stadi.
“Tunawaomba wazazi na walezi tusaidiane kwa pamoja katika harakati za kuwahamasisha wasichana kwani ndio tegemeo la jamii yetu,
No comments
Post a Comment