CCM YAFUTA NDOTO ZA SAMWEL SITTA RASMI,YAMPA BARAKA NDUGAI KUWA SPIKA,SOMA HAPO
![]() |
Mbunge wa Jimbo la Kongwa Ndugu Job
Ndugai akiongea na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa NEC baada ya jina lake
kupitishwa na wabunge wa CCM.
|
KAMATI ya Bunge ya Chama cha Mapinduzi (CCM) limempitisha bila kupingwa mgombea wa Uspika, Job Ndugai kugombea nafasi hiyo katika Bunge la 11, baada ya wagombea wenzake kujitoa.Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).
Ndugai alipishwa kwa kauli moja
baada ya wagombea wawili waliyojitokeza awali kujitoa na kulazimika kumpitisha
Ndugai ambaye alikuwa Naibu Spika wa Bunge la 10.
Wagombea
hao walikuwa ni Tulia Akson na Abdallah Ally Mwinyi huku ikielezwa kwamba
waliaamua kufanya hivyo kwa madai kuwa wanaamini Ndugai anauwezo wakufanya kazi
hiyo kutokana na uzoefu aliyoupata katika Bunge la 10.
Hata
hivyo, vyanzo vya ndani katika kamati ya bunge ya wabunge wa CCM inaeleza kuwa
Ndugai amepitishwa kuwania nafasi hiyo kutokana na wagombea wenzake
kushawishiwa kujitoa.
Chanzo
hicho cha kuaminika kililiambia MwanaHALISI Online kuwa baada ya kufika katika
ukumbi wa wa mikutano wa CCM Makao Makuu ‘White House’ aliyekuwa wa kwanza
kujieleza alikuwa Abdallah Ally Mwinyi, ambaye amesema kuwa licha ya kuwa na
nia ya dhati katika kuwania nafasi hiyo lakini ameamua kujitoa huku akidai kuwa
anamuunga mkono mwenzake ambaye ni Ndugai.
Chanzo
hicho kiliendelea kusema kuwa baada ya Dk. Tulia Akson kupewa nafasi ya
kujieleza, naye pia aliwaambia wajumbe kwamba kweli alikuwa na nia kubwa ya
kuwania nafasi hiyo ili aweze kuwa mmoja wa wabunge.
Mbali
na hilo chanzo chetu kinaeleza kuwa Dk. Akson alieleza kwamba alikuwa anatamani
kuwa miongoni mwa wabunge, kutokana na imani ya Rais kumteua na kuwa mbunge wa
viti maalumu hiyo ilimfanya ajitoe kwenye nafasi hiyo ya kuwania nafasi ya
uspika.
Hata
hivyo, Dk. Akson amesema kutokana na kuwa mbunge wa kuteuliwa kwa sasa anayo
shauku kubwa ya kuwania nafasi ya unaibu spika kutokana na kuwa yeye ni mmoja
wa wabunge tofauti na angekuwa nje.
Baada
kuteuliwa, Dk. Akson alijigamba kuwa ana matarajio makubwa ya kuwa mgombea
unaibu spika jambo ambalo linatajwa kwamba linaweza kumfanya aliyekuwa
Mwenyekiti wa Bunge la 10, Mussa Zungu.
“Kuna
uwezekano Zungu akajikuta katika wakati mgumu zaidi iwapo Dk. Akson atagombea
unaibu kwani kuna kila dalili za kutaka naibu Spika awe mwanamke ili kuendesha
bunge kwa usawa wa kijinsia,” kilisema chanzo cha habari wetu.
Kwa
upande wake katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema kamati ya bunge ya
CCM kwa kauli moja imempitisha aliyekuwa Naibu Spika wa bunge la kumi na mbunge
wa Kongwa Ndugai.
Hata
hivyo Nape hakuweza kufafanua ni kwanini wagombea wengine walijitoa na
kutokupigiwa kama ilivyo katika miaka yote.
“Hakuna
sababu bali wamejitoa kwa sababu wanamuamini Ndugai kwamba ana uwezo wa
kuviendesha vikao vya Bunge kwa kuzingatia kanuni,” amesema.
Nape,
amesema baada ya kupatikana jina hilo litapelekwa Ofisi za Bunge kwa ajili ya
kuteuliwa kuwa mgombea wa nafasi hiyo kwa kushindana na mgombea wa kambi ya
upinzani.
Kwa
upande wake Ndugai baada ya kupitishwa na chama chake ili kuwania nafasi ya
Uspika, amesema ataendesha bunge kwa viwango vya juu na tofauti na ilivyokuwa
kwa miaka yote.
Amesema
tangu Tanzania ipate uhuru, haijawahi kuwa na bunge kama bunge la kumi na moja
kwa kuwa bunge la sasa lina vijana wengi na wasomi wengi.
“Bunge
la 11 ni bunge ambalo lina vijana wengi ambao ni wasomi hivyo kutakuwepo na
changamoto kubwa katika Bunge hili ni kuhakikisha haki inatendeka kwa vyama
vyote kwa kuzingatia misingi ya kanuni.
“Nitawatendea
haki wabunge wote wa vyama vyote hapatakuwepo na uonevu wowote kwa mbunge
yoyote ambaye atakuwa akifuata kanuni na utaratibu wa kibunge,” amesema Ndugai

No comments
Post a Comment