NECTA YATOA IDADI YA WATAHINIWA WA KIDATO CHA PILI NA DARASA LA NNE,SOMA HAPO KUJUA
| Pichani nia Katibu mkuu wa baraza la Mitihani nchiniDkt Chalse Msonde akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es salaam |
BARAZA la Mitihani nchini (NECTA) limesema takribani wanafunzi 397,250
wameanza mtihani wa kujipima kwa kidato
cha pili katika shule 4,764 nchi nzima, kwaanzia leo tarehe 16 hadi novemba 27
mwaka huu.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Kati ya wanafunzi hao waliosajiliwa ,wavulana ni
197,452 sawa na asilimia 49.70 na wasichana ni 199,798 ambao pia ni sawa na
asilimia 50.30,
Sanjari na
hao pia watahiniwa 67 wasioona na watahiniwa wenye uoni hafifu ni 224 ambao
maandishi ya karatasi zao za mtihani hukuzwa.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,Katibu mkuu wa NECTA Dkt
Charles Msonde amesema maandalizi yote ya mtihani wa kidato cha pili
yamekamilika ikiwemo kupeleka vitendea
kazi katika shule zote nchini.
Dkt
Msonde amesema lengo la mtihani huo ni kuwapima uwezo na uelewa wa wanafunzi
katika yale yote waliojifunza kwa kipindi cha miaka miwili cha masomo yao.
Vilevile,Necta
pia imesema jumla ya wanafunzi 1,036,694 wamesajiliwa kufanya mtiani wa darasa
la nne kwa mwaka huu na mtihani huo unatarajiwa kufanyika tarehe 25 na 26
Novemba mwaka huu,
“Mtihani
huu wa darasa la nne waliosajiliwa kwa upande wa wavulana ni 501,714 sawa na
asilimia 48.40,na wasichana ni 534,980 sawa na asilimia 51.60”amesema Dkt
Msonde.
Pia amesema
kati ya hao,wapo watahiniwa wenye uoni hafifu ni 501 ambao maandishi ya
karatasi zao za mtihani hukuzwa pamoja watahiniwa wasio onaona 84.
Hata
hivyo,Dokta Msonde amewahasa wasimizi pamoja na wanafunzi kufuata kanuni na
sheria za mitihani na kucha mchezo mchafu wa kufanya udanganyifu.
“Baraza
halitasita kumchukulia hatua kali za kisheria mtu yeyote atakaye kiuka kanuni
za mitihani kwa kufanya udanganyifu,tunawataka wasimamizi na wanafunzi kuepuka
hali hii,kwa kufuata kanuni na taratibu za mitihani.”
No comments
Post a Comment