PIGO KWA SERIKALI YAACHAKAZWA MAHAKAMANI,NI KESI YA KAMANDA MAWAZO,SOMA HAPO KUJUA
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akizungumza na wananchi waliojitokeza nje ya mahamaka juu hatma ya kesi ya Alphonce Mawazo. |
NA KAROLI VINSENT
MZIMU wa Serikali kushindwa kwenye kesi nyingi
mahakamani ni kama umeanza kuendelea tena hata kwenye utawala mpya wa Serikali ya
Rais John Magufuli,
Ambapo baada ya leo serikali kuangushwa mahakamani
na Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema pamoja na Familiya ya aliyekuwa mwenyekiti wa
Chadema mkoani Geita,Marehemu Alponce Mawazo,
Taarifa kutoka Mahakama
kuu kanda ya Mwanza zinaarifu kuwa Familia ya Amri ya Jeshi la polisi kuwa Mawazo asiagwe Mwanza kwa kuwa kuna
hofu ya kipindupindu imetupiliwa mbali na Mahakama hiyo.
Mahakama hiyo iliyoketi chini ya Jaji Lameck Mlacha imetoa
ruhusa mwili wa Alphonce Mawazo kuagwa jijini Mwanza na imeagiza Jeshi la
Polisi kutoa Ulinzi siku hiyo lakini Ulinzi huo usivuke mipaka.
Sehemu ya hukumu ya kesi hiyo inasema "Kazi ya Polisi ni
kulinda raia na si kuzuia mazishi.."
Hakuna maoni
Chapisha Maoni