WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWATOA HOFU WALIMU WOTE NCHINI,SOMA HAPO KUJUA
WAZIRI mkuu,Kasim Majaliwa amesema adhima ya
Serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha inawawekea mazingira mazuri walimu
ikiwemo kuongezea mishahara pamoja na vitendea Kazi vya kufundishia.Andika
KAROLI VINSENT,endelea nayo.
Wazari mkuu Majaliwa ameyasema hayo leo jijini dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa uuzaji hisa za Benki ya walimu,MCB kwenye soko
la hisa mkoani Dar es Salaam,(DSE) ambapo Majaliwa amesema licha ya kukaa kwa mda mrefu
kwenye wizara ya TAMISEMI ambayo inasimamia masuala ya elimu imemfanya kuzijua shida wanazozipata
walimu na kuhaidi kupambana nazo.
,
“Nahafamu fika matatizo ya walimu tangu nikiwa
TAMISEMI,hata Rais John Magufuli amehaidi kwenye hutuba yake Bungeni ni kwamba
awamu ya tano itaweka mbele suala la maslahi ya walimu ili kuhakisha kila
mwalimu anapata kipato kizuri pamoja na vitendea kazi”amesema Waziri mkuu
Majaliwa.
Amesema hatua ya Chama cha Walimu,CWT kuanzisha
Benki ya walimu na mpaka kufikia hatua ya kuanza kuuza hisa zake DSE ni jambo
jema linalofaa kupongezwa kwani amedai ujio wa Benki ya walimu itakuwa ni
chachu ya kuwasaidia walimu kwenye masuala mbali mbali,..
Kwa upande wake Afisa mtendaji mkuu wa DSE,Moremi
Marwa amesema mpaka sasa makampuni
yaliyoorodheshwa katika soko hilo yamefikia
22,
Ambapo amedai kipindi cha miaka mingi soko la hisa
limekuwa likitoa mwongoza mzuri kwa makampuni ya ndani pamoja na serikali
katika kuzisimamia hisa zake
Hakuna maoni
Chapisha Maoni