MBUNGE SAED KUBENEA AIBUA UFISADI WA KUTISHA MANISPAA YA KINONDONI,AANZA MAKEKE YAKE SASA,SOMA HAPO KUJUA
Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea akizungumza na wakazi wa jimbo hilo |
MBUNGE wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea ameibua
ufisadi wa Shilingi bil. 1.2 kwa mwaka katika Halmashauri ya jiji la Dar es
Salaam unaofanywa kupitia ufuaji wa majoho ya madiwani. Anaandika Josephat Isango …
(endelea).
Kubenea amesema hayo Stendi Kuu
ya mabasi yaendayo mikoani alipofanya ziara ya siku moja kutembelea soko la
Urafiki maarufu kama Mahakama ya ndizi, soko la Mabibo na kuhitimisha ziara
yake katika Stendi za Ubungo na Simu 2000
“Baada
ya kufanya uchunguzi tumebaini kuwa mradi huo wa ufuaji majoho kabla ya
madiwani kufanya kikao unaotumia shilingi bilioni 1.2 hivyo basi Halmashauri ya
Manispaa itakayokuwa chini ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) tukianza kazi
tutaufuta,” alisema Kubenea.
Aliongeza
kuwa kufutwa kwa mradi huo kutafanywa mara moja baada ya Ukawa kupata Meya wa
Manispaa na Jiji kutokana na ukweli kwamba wana Halmashauri mbili kati ya tatu
hivyo zitawawezesha kumpata Naibu Meya katika Chama Cha Wananchi (CUF) na Chama
Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Kubenea
alisema jambo jingine ambalo watakalolisimamia ni kuhakikisha wanaondoa
Mahakama ya jiji kwa sababu wamegundua hakuna mahali popote katika bara la
Afrika.
“Mahakama
hiyo ni ya kikoloni kwani hakuna mahali popote katika bara la Afrika ambako ipo
zaidi ya Tanzania kwenye jiji la Dar es Salaam, hivyo ili kuwaokoa mama lishe,
madereva bodaboda, machinga ni lazima tuhakikishe Mahakama hiyo tunaifuta,”
alisema Kubenea.
Mbunge
huyo alisema wamedhamiria kwenda kufuta zuio madereva wa bodaboda kuingia mjini
lililokuwa limewekwa chini ya aliyekuwa Meya wa jiji, Dk. Didas Masaburi ili
kuwawezesha vijana hao kufikia katika mji huo
Habari hii kwahisani ya Mwanahalisi oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni