Zinazobamba

KOVA AFUMUA IDARA TRAFICK DAR,PIA ANASA WAHAMIAJI HARAMU 105 KUTOKA NCHINI ETHOPIA,SOMA HAPO KUJUA


Pichani ni Kamisha wa Kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewabadilisha kazi wakaguzi  7 na askari wa vyeo mbali mbali wa kikosi cha usalama barabarani kutokana na kukiuka kanuni za kazi.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo,
Akizungumza  leo na Waandishi wa Habari Kamishna wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova  amesema umamuzi wa kuwabadilisha askari hao kutoka kikosi cha usalama barabarani kwenda kazi nyingine mbali mbali za kawaida umetokana  na ufuatiliaji wa mienendo yao na kubainika sio mizuri, Kamishna Kova ameitaja mienendo hiyo mibaya ni matumizi ya lugha ya matusi,kuomba rushwa,kuchelewa kazini pamoja kutumia vilevi nyakati za kazi, 
 Amesema mbali na kufuatilia na kubaini matendo hayo kwa askali hao,pia Kamishna Kova amesema mara kwa maramara wananchi wamekuwa wakiwalalamika askali hao kufanya kazi kinyume na sheria za nchi.
Hata hivyo Kamisha Kova amesema hatua ya kuwabadilisha kazi Askali hao si ya kwanza tu kwani  bado uchaguzi unaendelea kufanyika kwa wale ambao wataendelea kufanya kazi chini ya viwango.
Katika hatua Nyingine Jeshi hilo limewakamata wahamiaji haramu wapatao 105 kutoka nchini Ethopia,
Kamisha Kova amewaambia wanahabari kuwa wahamiaji haramu hao walikamatwa maeneo ya Tabata Segerea ilala Jijini Dare s Salaam, 
 Ambapo Jeshi hilo lilipata taarifa kutoka kwa wasamaria wema juu ya uwepo wa watu hao,ndipo Jeshi hilo lilipofuatilia taarifa hizo pamoja na kufanya msako kwenye nyuma moja ambayo ilitajwa na wasamaria wema hao na kukuta waamiaji hao 105,

 Kamishna Kova amesema kuwa baada ya uchunguzi wa awali uliofanywa na Jeshi hilo wakabaini watu hao walikuwa chini ya usimamizi wa mtu mmoja aitwaye Zainabu Uwinza,miaka 25 ambaye inasemakana ni raia wa Burundi ambaye amekuwa anahusika na  biashara ya usafirishaji binadamu kutoka nchi za Afrika kwenda ulaya kwa pesa za kimalekani Dolla 1000.

Hakuna maoni