Zinazobamba

SAMWELI SITTA KUIPASUA CCM TENA,SAKATA LAKE LA KUFIA KWENYE USPIKA WA BUNGE LIJALO LAZIDI IBUA UTATA,SOMA HAPO KUJUA

Samwel Sitta akijaza Fomu ya Uspika leo Katika Ofisi ndogo ya CCM iliyoko Lumumba na kushuhudiwa na Ndugu Seif khatibu

SAMWEL Sitta anaweza kukipasua tena Chama cha Mapinduzi CCM kutokana harakati za kuutaka Uspika wa Bunge la 11.Mtandao huu umebaini.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
     Taarifa za kuaminika ambazo mtandao huu umezipata kutoka ndani ya CCM pamoja na wanaojiita ni wapambe wa Sitta wamesema Mwanasiasa huyo amepania kufa na kupona ili kuhakikisha anakuwa spika wa Bunge hilo linatorajiwa kuanza Jumanne ya wiki ijayo.
     “Ninachokwambia ndugu huyo Sitta na hatua yake hii ya kujiapiza anautaka Uspika kwa udi na uvumba nakwambia anakiingiza tena chama hichi matatizoni ndugu,yaani chama kilipasuka wakati wa mchujo wa Urais,lakini tumepambana na kurudisha chama hichi kwenye usawa lakini huyu mtu anataka kukipasua chama chetu na tamaa yake ya madaraka”amesema kiongozi mmoja mwandamizi wa CCM.
        Taarifa kutoka Lumumba zinasema teyari mpaka leo jioni saa kumi makada mbali mbali wa chama hicho wamejitokeza na kuchukua fomu ya kuwania Uspika.
      Makada hao  ni yeye Samweli Sitta,Aliyekuwa Mbunge wa Karagwe,Gasbert Blandes,leonce Mulenda,Georgy Nangale,Profesa Costa Mahalu,
     Wengine ni Muzamil Kalokola,Bunda Sonoko,Simoni Rubugu.   
      Sitta ambaye alikuwa Spika kwenye Bunge la Tisa na pia akabahatika tena kuwa Mwenyekiti wa Bunge lilokuwa na Katiba  ambapo Sitta anatuhumiwa kwa kitendo chake cha kuendesha Bunge hilo la Katiba kwa ubabe huku akidaiwa kuhusika katika kufanya udanganyifu wakati wa kupata akidi ya 2 ya tatu ya wajumbe kutoka Zanzibar,
     Sanjari na hilo pia Sitta analahumiwa pia kuhusika katika kuwatolea maneno ya Kebehi viongozi wa dini hasa Maaskofu pale walipokuwa wanamtaka afuate maoni ya iliyokuwa Tume Jaji Warioba.
      Mbali pia na Bunge la Katiba pia Samweli Sitta inadaiwa kulingiza Taifa kwenye hasara kubwa kutokana na kipindi kile alipokuwa Spika wa Bunge la Tisa,
       Ambapo inaelezwa Azimio Na 13 la Bunge Juuu ya Mkataba tata kati ya serikali na Kampuni ya kufua Umeme wa dharula ya Richmond Development Company (RDC)  ililitaka wazi serikali iweke mikataba yote wazi bungeni ili kila mwananchi aione na kuweza kuondoa mianya ya kifisadi.
         Lakini wakati wa kijadili maazimio 23 yaliyojadiliwa na kamati Teule iliyoundwa kuchunguza mazingira ya udanganyifu katika mkataba huo,Samwel Sitta alisimamia kidete na kutaka  Mamlaka ya Juu kuhamua suala hilo.
    Kitendo hiko cha Sitta kufanya hivyo ndio kimefungua Mwanya kwa watendaji wengi wa serikali kutumia fursa hiyo kuingia kwenye mikataba ya kifisadi kwa kisingizia cha usiri .
     Azimio lilikuwa linapiga marufuku serikali kuendelea na kile kilichoitwa ni “Utaratibu uliorithiwa  kwa wakoloni na kujigeuza kuwa mazoea wa kuzuia mikataba ya kibiashara kuwekwa wazi hata kwa walipa kodi wenyewe.
         Bunge lilitaka mikataba yote ya Madini,Gesi,Mafuta,ununuzi wa mitambo na mingine  ambayo watendaji wa serikali wanaingia kwa niaba ya nchi ifikishwe bungeni ijadiliwe,ilidhiwe na kuidhinishwa.
       Duru mbalimbali zinasema “kama sio sitta kusitisha mjadala kabla ya bunge kuing’ang’aniza serikali leo kusingekuwa kichaka cha kuficha mikataba yote ya serikali.
     “Spika sitta alikatiza mijadala kuichia mamlaka na mamlaka imekataa kuchukua hatua na hapo ndipo tulipofikia tunafichwa mikataba”
         Hadi Sitta anafunga mjadala huo wa Richmond Bungeni agizo hili alikutekelezwa ,jambo ambalo limetoa mwanya kwa  kwa serikali kuendelea kufanya mikataba kuwa ya siri.
 Madai kuwa maamuzi ya Sitta kuhusu Richmond yanaendelea kuliangamiza taifa ,yameibuka wakati Kamati ya kudumu ya Bunge ya Mashirika ya Umma (PAC),ikikwaruzana na shirika la Petroli Tanzania (TPDC) kuhusu Mikataba ya Gesi




No comments