CCM WATUMIA MBINU KAMA WALIYOTUMIA KWA LOWASSA KUMKWAMISHA SAMWEL SITTA KWENYE USPIKA,WARUHUSU MAKADA WAKE LUKUKI KUCHUKUA FOMU ZA USPIKA,SOMA HAPO

CHAMA cha Mapinduzi CCM kimelazimia kutumia njia
iliyotumika kamkata aliyekuwa Kada wa chama hicho Edward Lowassa wakati wa
kinyang’anyilo cha kupata nafasi ya Urais,ambapo sasa inatumika katika kumkabili pia Samwel Sitta
kwenye nafasi ya kuwania Uspika.Mtandao umedokezwa.Anaandika KAROLI VINSENT
endelea nayo.
Taarifa
za kuaminika katoka Ofisi ndogo ya CCM iliyoko Lumumba Jijini Dar es Salaam,zinasema kwa sasa chama
hicho kimelazimika kutumia mbinu hiyo ili "kumzima" Sitta katika harakati zake za
kutaka Uspika wa Bunge lijalo linatarajia kuanza wiki ijayo ili kukiepusha chama
hicho kuingia kwenye mapasuko tena.
Mbinu
hiyo inayotajwa ni ile ya kuwaruhusu makada wengi wa chama hicho pamoja na
wabunge wateule kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu ya Uspika ili wakati wa
Kamati kuu ya CCM itakapokata jina la Sitta ,ili iwe rahisi kujibu mapigo ya
Sitta atakapolalamika.
“Ujue
sahivi chama kimeshabaini mbinu za Sitta,sahivi tumewaruhusu makada wengi
wachukue fomu ili tumkabili huyu bwana (Sitta) maana ameshaanza kuweka mikwala
mingi ambayo itaweza kukigawa chama chetu,na hii mbinu itasaidia wakati Sitta
analalamika tutamjibu mbona wenzako wamekatwa inakuwaje alalamike yeye”
Mpaka
mtandao huu unaripoti habari hii ni teyari makada ishirini, wamejitokeza na
kuchukua fomu ya uspika ambao kwa siku ya jana walichukua makada 10,
Kwa
mujibu wa Chanzo chetu kilichopo Lumumba kimesema kwa siku ya leo wamejitokeza makada kumi kuchukua fomu hizo,
Makada hao
ni Julias Pawatila,na Aliyekuwa naibu spika wa bunge la kumi Job Ndugai,Dr
Tulia Acksoni,Mwakalika Watson,
Wengine
ni Dk Didas Massaburi,Dk Medad Kalamani,Lita Mlaki,Veraikunda Urio.
Mbinu hiyo inayotajwa kusukwa kwa ustadi mkubwa na
Kiongozi mmoja mwandamizi wa
Serikali,mbinu hiyo ambayo ilitumiwa wakati wa kulikata jina la Lowassa ndani ya CCM
baada ya kuwaruhusu makada wengi
kuchukua fomu ambao makada zaidi ya 32 walijitokeza kuchukua fomu za Urais ndani
ya chama hicho.
Hata Lowassa alipohoji uharali wa kamati
kuu kukata jina lake mara kwa mara viongozi wa CCM walijitokeza na kusema iweje
alalamike yeye wakati makada wengi walijitokeza kuchukua fomu na
hawakulalamika.
No comments
Post a Comment