NEC YAMALIZA UBISHI,YATANGAZA RASMI IDADI YA MADIWANI WA VITI MAALUM,SOMA HAPO KUJUA
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC
Bw. Kailima Ramadhani akizugumza na waandishi wa
habari (hawapo pichani) juu ya viti maalumu vya Udiwani ambavyo Madiwani
wake wameteuliwa na Tume hiyo ni viti 1393, kutoka katika Vyama vya
CCM,CHADEMA,NSSR-MAGEUZI pamoja na CUF.Mkutano huo umefanyika leo jijini Dar es
Salaam ,Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Huduma za Sheria wa NEC Emmanuel Kawishe.
|
TUME ya Taifa ya Uchaguzi( NEC)
imesema hadi sasa viti maalumu vya Udiwani ambavyo Madiwani wake wameteuliwa na
Tume hiyo ni viti 1393, kutoka katika Vyama vya CCM, CHADEMA, NSSR-
MAGEUZI pamoja na CUF.
Hayo yamesemwa leo Jijijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Uchaguzi kutoka NEC Bw. Kailima Ramadhani wakati akitoa taarifa kwa Umma kuhusu uteuzi wa madiwani wanawake wa V iti Maalumu.
Aidha Bw.Ramadhani amesema kuwa idadi ya Viti maalumu Vya Udiwani ni 1,408 nakwamba kutokana na majimbo nane na kata thelathini na Nne ambapo Uchaguzi haujakamilika kwa Sababu mbalimbali, hatua hiyo itasababisha kubakia viti 15 ambavyo vitagawanywa mara baada ya Uchaguzi kukamilika ili kufikia idadi ya viti 1,408 kutoka viti 1393 vinavyo tambulika kwa sasa.
Aidha amefafanua kuwa kutokana na Viti hivyo Maalumu Vya Udiwani Vilivyoteuliwa na NEC, Chama Cha Mapinduzi CCM kimepata viti 1,022,Chama Cha Demokrasia na Mawendeleo CHADEMA 280,Chama Cha Wananchi CUF-79, ACT WAZALENDO viti 6 pamoja na NSSR MAGEUZI viti 6.
Amesema kuwa tume imeamua kutoa taarifa ya uteuzi wa viti maalumu Vya Udiwani Nchi nzima ya Madiwani waliyoteuliwa na Tume kutokana na Kanuni za Kudumu za Mikutano ya Halmashauri, Mabaraza ya Madiwani yanatakiwa kuitishwa siku thelathini tangu tarehe ya Uchaguzi ifanyike

Katika hatua Nyingine Mkurugenzi huyo
wa Uchaguzi NEC amesema kuwa mwisho wa Uchaguzi katika Majimbo na
Kata ambazo hazikufanya Uchaguzi ni Desemba 20 mwaka huu, ambapo katika jimbo
la Uranga Mashariki pamoja na Lushoto uchaguzi utafanyika Novemba 22 mwaka
huu,nakuwaomba Wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura ili kuchagua
kiongozi wanaomtaka.
No comments
Post a Comment