MKURUGENZI WA TUME YA UCHAGUZI ATANGAZA MAJINA NA MADIWANI WA VITI MAALUM
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi Ndugu Ramadhan Kailima akitangaza majina ya Madiwani wa Viti
Maalum walioteuliwa na tume ya uchaguzi kutoka vyamba mbalimbali vya
siasa vilivyoshiriki uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani
uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu nchini kote kutokana na idadi ya
ushindi wa viti vya wabunge na madiwani kwa Chama husika.
Bw. Kailima ametanganza majina
hayo wakati alipokutana na waandishi wa habari leo kwenye ofisi za Tume
hiyo zilizopo jengo la Posta mkabala na Wizara ya Mambo ya Ndani.
…………………………………………………………………………..
NA SHAMIMU NYAKI- MAELEZO
Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania ( NEC)
leo imetangaza majina ya Madiwani wa viti maalum walioteuliwa na vyama
vyao vya siasa kufuatia Uchaguzi Mkuu uliofanyika Octoba 25 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari katika
ofisi za Tume hiyo, Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Tanzania Bw.
Ramadhani Kailima amesema jumla ya viti maalum vilivyopo ni 1407 kutoka
Kata 3923 cha Uchaguzi, ambapo viti 1393 ndivyo vilivyogawiwa kwa vyama
vya siasa vilivyoshiriki Uchaguzi na kutimiza vigezo vya kupata Madiwani
wa viti maalum.
Aidha katika mgawanyo huo Chama Cha
Mapinduzi (CCM) kimepata viti 1,022 kikifatiwa na Chama Cha Demokrasia
na Maendeleo ( CHADEMA) viti 280 huku Chama Cha Wananchi CUF kikipata
viti 79,ACT Wazalendo na NCCR-Mageuzi wakipata viti 6 kwa kila chama.
Ameongeza kuwa idadi kamili ya viti maalum
itakamilika pale Uchaguzi katika Kata ambazo hazikufanya uchaguzi
kukamilika na pia ameviagiza vyama vya siasa kukamilisha uwasilishaji
wa majina ya waliowateuwa kuwakilisha Kata zao katika Uchaguzi Mkuu
uliopita ili waweze kusajiliwa.
“ Waandishi muache malumbano ya mambo ya
vyama vya siasa bali muhimize wananchi kujitokeza kupiga kura katika
uchaguzi unaoendelea nchini ili kutimiza haki yao ya msingi ya kikatiba”
alisema Bw Kailima.
Uchaguzi kwa majimbo ambayo
hayakuweza kuwapata wawakilishi wao yanatarajiwa kufanya uchaguzi hivi
karibuni. Majimbo hayo ni Lushoto, na Ulanga Mashariki ambao
utafanyika tarehe 22 Novemba,mengine ni Ludewa na Masasi mjini
utakaofanyika tarehe 20 Desemba na jimbo la Kijitoupele huko Zanzibar
utafanyika hapo baadae.

No comments
Post a Comment