WIZARA YA NISHART YAISHUKIA TANESCO KWA WATEJA WANAOIBA UMEME,SOMA HAPO KUJUA
pichani ni Afisa habari kutoa Wizara ya Nishart na Madini,Badra Masoud katika ukumbi wa habari maelezo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akitoa taarifa yake kuhusu wizi wa Umeme |
IKIWA ni dalili za Serikali ya Rais Joh Magufuli
kuanza kukusanya kodi kwa kubana mashitika ya umma ni kama imeanza baada ya
SERIKALI kuliagiza shirika la TANESCO kuimarisha kikosi chake cha ukaguzi wa
watumiaji wa umeme ili kubaini wateja wasio waaminifu wanaoiba umeme pamoja na
kuwachukulia hatua za kisheria. Anaandika KAROLI VINSENT ...
(endelea).
Hayo yamesemwa leo na msemaji
wa Wizara ya Nishati na Madini, Badra Masoud katika ukumbi wa habari maelezo
Jijini Dar es Salaam alipokuwa akitoa taarifa yake kuhusu wizi wa Umeme.
Masoud amesema wizara yake
inatarajia kuunda kikosi maalum kitakachojumuisha wataalam kutoka TANESCO na
vyombo vya usalama kwa lengo la kukabiliana na tatizo hilo linalokosesha mapato
shirika la TANESCO.
Amesema kuwa sambamba na
kulitaka shirika hilo kukabiliana na wizi wa umeme, amezitaka pia taasisi
mbalimbali za Serikali na zisizo za Serikali kuzingatia matumizi bora ya Umeme
ili kudhibiti upotevu wa nishati hiyo muhimu. Utaratibu huo pia hufanywa na
nchi nyingi Duniani kwa lengo la kukabiliana na upotevu wa umeme.
Masoud ameeleza kuwa hatua
hiyo imekuja baada ya taasisi kuona kwamba taasisi mbalimbali huwa zinaacha
umeme ukiendelea kupotea baada ya muda wa kazi.
Ameya horodhesha baadhi ya
matumizi hayo ya vifaa ambavyo huviacha vikiendelea kufanya kazi hata kwa muda
ambao sio wa kazi, kama vile AC, taa, kompyuta na baadhi ya vifaa vingine
vinavyotumia umeme.
Akizungumzia hali ya umeme
hapa nchini, Masoud amesema hakuna mgawo wowote unaoendelea hivi sasa kwani
hali ya uzalishaji ni nzuri pamoja na mabwawa ya maji ambayo hutumika kuzalisha
umeme kukauka lakini kiasi kikubwa cha umeme kinachozalishwa kwa sasa
kinatokana na Gesi asilia ambapo kiasi kidogo kinazalishwa kwa kutumia mabwawa
ya maji.
“kiasi cha umeme
kinachopatikana kwasasa ni megawati 1500 huku matumizi ikiwa ni kati ya
megawati 800 na 900 kwa siku.” Amesema Masoud.
No comments
Post a Comment