NDUGAI AULA USPIKA RASMI,WANANCHI WAMTAJA MWAKYEMBE UWAZIRI MKUU,SOMA HAPO KUJUA

WAKATI Bunge la 11 likiwa limekwishapata Spika, Job
Ndugai, jina la Dk. Harrison Mwakyembe limeendelea kupewa nafasi ya kuwa Waziri
Mkuu wa Serikali ya Awamu ya Tano inayotarajiwa kutangazwa hivi karibuni. Anaandika Dany Tibason, Dodoma …
(endelea).
Ndugai ambaye alikuwa naibu
spika wa Bunge la 10, amefanikiwa kushinda kiti cha Spika katika Bunge la 11
baada ya kushinda kura 254 ambazo ni sawa na asilimia 70 ya kura zote.
Kinachosubiriwa sasa ni uteuzi wa Waziri Mkuu wa Serikali ya awamu ya tano
ambapo Dk. Mwakyembe akitajwa.
Wakizungumza
na MwanaHALISI Online, baadhi ya wananchi wamesema kutokana na Taifa
lilipofikia, linahitaji waziri mkuu ambaye atafanya kazi bila ya kupokea
maelekezo kutoka kwa baadhi ya vigogohttps:.
Kaimu
Katibu Mkuu wa Chama cha Chausta, Amina Mcheka, amesema kutokana na Mwakyembe
kutajwa kwenye mitandao ya kijamii mbalimbali, anaona anafaa kuwa kuwa waziri
mkuu.
Amesema,
serikali ijayo inahitaji waziri mkuu ambaye ataendana hali halisi ya jiografia
ya nchi, kwa ajili ya kukimbizana na umasikini wa watanzania.
Amina,
amesema kuwa na mtu anayefaa kuwa waziri mkuu katika serikali ijayo ni Dk.
Mwakyembe kutokana na wananchi kuamini kuwa ni mchapa kazi, ambaye hana hana
maamuzi ya woga katika kutetea masilahi ya wananchi.
“Siyo
kama mawaziri wakuu waliyopita hawakufanya kitu, bali hivi sasa tunahitaji
waziri mkuu ambaye atafanya kazi kwa ufanisi na atakayendana na kauli mbiu ya
Rais inayosema Hapa Kazi Tu,” amesema Amina.
Amina,
amesema anatambua kuwa nafasi ya uwaziri mkuu inatokana na kuteuliwa bado
anaamini mawazo ya wananchi yananafasi kutokana na kufahamu utendaji wa baadhi
ya viongozi serikalini.
Hatibu
Yahya, amesema, licha ya Dk. Mwakyembe kuwa chaguo la baadhi ya wananchi bado
haamini kama Adad Rajab ambaye ni Mbunge wa Muheza atapenya kwenye nafasi hiyo
ingawa akipewa anaweza.
“Unajua
kama angekuwa amefanya kazi ya uwaziri kwa vipindi vyote viwili nadhani hicho
kingekuwa kigezo kizuri, ambacho kingemuongezea uwezekano wakupata nafasi
hiyo,” amesema Yahya.
VEDEO YAKE HII HAPA
VEDEO YAKE HII HAPA
Amesema
nafasi kubwa ambayo inamfaa Adad katika Baraza la Mawaziri lijalo ni ile ya
Mambo ya Nchi za Nje, kwani hiyo inatokana na uzoefu wake wa kufanyakazi za
ubalozi nchi za nje.
Naye
Mchungaji Wiliam Mwamalanga, amesema kuwa taifa linahitaji waziri mkuu mwenye
hekima ya mungu ya uongozi ambaye atamsaidia Rais kuiangalia jamii ya watu wa
kipato cha chini kabisa.
“Tunataka
waziri mkuu ambaye ataondoa makundi ya uhasama na kuleta utulivu ndani ya nchi
kama atapatikana ambaye hana maadili kuna hatari nchi itawaka moto jambo ambalo
hatuliombei,” amesema Mchungaji Mwamalanga.
Mchungaji
Mwamalanga, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili, Amani na Haki za
Binadamu wa Madhehebu ya dini ya Kiislam na Kikristu, amesema pia awe mtu
asiyekurupuka.
“Tunataka
waziri mkuu asiyekurupuka, atakayekuza uhuru wa wa habari, atakayeisimamia
serikali na kurudisha maadili ya umma na kuiweka serikali mikononi mwa wananchi
ukilinganisha,” amesema Mchungaji Mwamalanga.
Alisema
katakuwa hana maadili atakuwa ni waziri mkuu ambaye ataimarisha makundi ya
mafisadi ambayo yataharibu nchi, kwa sababu mafisadi hao wataongeza gepu la
waliyonacho na wasiyonacho.
Hata
hivyo, Dk. Mwakyembe juzi, alikaririwa na vyombo vya habari akisema kuwa
kisheria uwaziri mkuu hauji kwa mtu kupitia kwenye mitandao ya kijamii kama
wananchi wanavyofikiria.
Mmoja
wa wananchi, Dk. Rex Kidyalla amesema kamwe haiwezekani kupatikana waziri mkuu
wa tofauti na serikali ya CCM kwani vongozi wanaotokana na chama hicho wote
wana akili zinazofanana.
“Unajua
watanzania hatuchagui viongozi na wala hatuchagui viongozi ikumbukwe kuwa nchi
hii wanaochagua viongozi ni watu watatu tu, mmoja ni Ally Hassan Mwinyi,
Benjamini Mkapa na Jakaya Kikwete, kwa mfumo huo hata sisi wananchi tukiwa na
mapenzi ya kumtaka waziri mkuu ambaye anaweza kufanya kazi za wananchi
haiwezekani kumpata.
“Hadi
sasa ni wazi kwamba viongozi wengi wanachaguliwa na viongozi wa ngazi ya juu
kwa maana hiyo inaonesha wazi kuna mtu ambaye ameshapangwa kwa ajili ya kushika
nafasi hiyo ambaye tayari atakuwa Waziri Mkuu hata kama tutapiga kelele
haitasaidia,” amesema.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi wa taasisi za elimu (THTU),
Dodoma Nashon Maisori amesema kwa sasa taifa linahitaji waziri mkuu mwenye
uthubutu, uadilifu,nuzoefu na awe kiongozi mwenye hekima.
“Mtu
mwenye sifa hizo ambaye anatakiwa kuwa waziri mkuu ni Dk. Harrison Mwakyembe,
huyu bwana amekufa na kufufuka haogopi tena, kwa CCM ilivyo sasa haina watu
wenye vigezo vya kuwa mawaziri.
“Nalazimika
kuona kuwa Dk. Mwakyembe kuwa waziri mkuu, kiongozi huyo aliweza kulipua mambo
mengi ambayo yalitikisa nchi, kama kweli Rais Magufuli anataka mtu mchapa kazi
na asiye ogopa mikikimikiki basi bila shaka ni Dk. Mwakyembe ila kwa watu ambao
wapo CCM tukizungumzia sifa ya uchafu hakuna aliye msafi,” amesema Maisori.
Kwa
upande wa viongozi wa dini ambao walitoa maoni yao nao wasema waziri mkuu
asipatikane kwa shinikizo la watu au baadhi ya viongozi bali jambo pekee
ateuliwe kiongozi ambaye ni mchapakazi na mwadilifu.
Akitoa
maoni yake Askofu wa Kanisa na Menonite Jimbo la Dodoma, Amos Muhagachi amesema
waziri mkuu ambaye anaweza kupatikana ni yule mwenye sifa ya kuongoza nchi bila
kuwa na ubaguzi wa aina yoyote.
“Mimi
siwezi kuwa mpiga ramli kwa kusema waziri mkuu awe mtu wa aina gani bali jambo
pekee Rais atumie hekima na busara kubwa kumpata kiongozi ambaye ni mchapa kazi
asiyekuwa na tabia ya kulipiza visasi au kulenga kujinufaisha,” amesema Askofu
Muhagachi.
Naye
shekhe wa mkoa wa Dodoma, Mustafa Rajabu amesema waziri mkuu anatakiwa kuwa ni
mtu ambaye anajitambua na kuwatambua watu ambao anawaongoza.
Kwa
upande wao waendesha bodaboda nao wameonekana kugawanyika huku wakisema
serikali haiwezi kuwa na waziri mkuu ambaye ni tofauti na wale waliopita
kutokana na mfumo uliopo kwa sasa ndani ya serikali.
Hali
ya mji wa Dodoma kwa sasa imeonekana kuwa na shamrashamra nyingi kutokana na
uwepo wa wageni wa wabunge ambao wanaendelea kuapishwa.
No comments
Post a Comment