KUMEKUCHA MANISPAA YA KINONDONI,UBOMOAJI KUANZA IJUMAA RASMI,SOMA HAPO KUJUA
| Pichani Mkutano wa Wizara ya Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi na Waandishi wa Habari kuhusu zoezi la ubomoaji wa
nyumba Manispaa ya Kinondoni (kuanzia kushoto) Mhandisi wa Manispaa ya
Kinondoni, Bw. Baraka Mkuya, Kamishna wa Ardhi Tanzania Dkt. Moses Kusiluka na
Kamishna wa Ardhi Msaidizi kanda ya Dar es salaam Bw. Methew Nhonge |
WIZARA ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi
imesema itaanza kuzibomoa nyumba zote zilizojengwa kiholela katika maeneo ya
Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam,Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Akizunguma na waandishi wa habari leo jijini
hapa,Kamishna wa Ardhi kutoka wizara ya Ardhi,Dk Moses Kusiluka amesema zoezi
hilo la ubomoaji nyumba hizo litaanza ijumaa ya terehe 18 ya mwezi huu
hadi tarehe 20 ya mwezi huu pia,
“zoezi hili la ubomoaji litaendeshwa na na manispaa ya kinondoni na wizara ya Ardi itasimamia
sera za ardhi na utaratibu za uendelezaji kuhakikisha zinafuatwa na kila
mmiliki wa ardhi”amesema Dk Kusiluka.
Dk Kusuluka
ameongeza kuwa uboaji huo utahususisha nyumba zote zilizojengwa bila kufuata
michoro ya upimaji miji,kibali na ujenzi pamoja na kutofuata matumizi ya maeneo
ya wazi.
Amedai
Wizara yake inafuata tamko Na 6.61 la sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995
ambayo inaitaka serikali kuhakikisha kwamba maeneo yote ya mjini yaliyotengwa
kwa shughuli za umma yanatumika kwa shughuli zilizokusudiwa na yalindwe
yasivamiwe.
Kwa
upande wake Mhandishi wa Manispa ya kinondoni,Eng, Baraka Mluya ameyataja
maeneno ambayo yatakumbana na Ubomoaji huo ni Mbezi,Tegeta,Bunju.Mwenge na
kinondoni Biafra.
Hata
hivyo Eng Mluya amewataka wananchi
kufuata taratibu za Ardhi ili kujiebuka na kadhia za kubomelewa nyumba.
No comments
Post a Comment