KUBENEA ATOA AHADI NZITO KWA WANANCHI WAKE,SOMA HAPO KUJUA
![]() |
Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea akiwa na wapiga kura wake |
MBUNGE
wa Ubungo na Mkurugenzi wa Hali Halisi Publishers, Saed Kubenea (Chadema)
amewahakikishia wakazi wa jimbo la Ubungo kuwa atawapatia maendeleo katika
jimbo hilo.Anaandika Dany Tibason, Dodoma …
(endelea).
Mbali na hilo amewapongeza
waandishi wa habari kwa kushirikiana naye katika kufichua maovu ambayo
yalipangwa kufanywa na serikali ya CCM kuwapora wapinzani ushindi.
Kubenea
alitoa kauli hiyo jana mjini hapa baada ya kuapishwa kuwa mbunge wa jimbo hilo
alipokuwa akizungumza na wananchi wa Ubungo zaidi ya 500 waliomsindikiza kwa
ajili ya kushuhudia jinsi anavyoapishwa.
Kubenea
akizungumza na umati wa wananchi hao amesema katika jimbo hilo atapambana na
wafanyakazi wazembe na legelege.
“Natangaza
kuwa wakurugenzi ambao wanasababisha uzembe na kudorora kwa maendeleo hakika
tutapambana nao ili kuondoa dhana ya kulindana.
“Tutaunda
halmasahauri yenye nguvu ambayo lengo kubwa ni kuhakikisha maendeleo
yanawafikia wananchi wote bila juwepo kwa ubaguzi,” amesema Kubenea.
Akizungumzia
suala la madereva bodaboda, amesema baada ya kuunda halmashauri madereva wa
bodaboda watatungiwa sheria ya kufika katikati ya mji tofauti na ilivyo sasa.
“Hatuwezi
kukubali kuona vijana wetu wakihangaika wakati wanatakiwa kuwezeshwa kufanya
kazi zao kwa ajili ya kujipatia kipato,” amesema Kubenea.
Pamoja
na mambo mengine Kubenea amesema yeye amefika bungeni kutokana na nguvu ya
umma, hivyo hatapandisha mabega kwa kuwabeza wananchi.
Akizungumzia
kuhusu kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo
(Chadema), Kubenea amesema ni jambo la kulaaniwa kwa kifo chake ambacho
kinahusishwa na wafuasi wa CCM.
No comments
Post a Comment