KASSIM MJALIWA AULA UWAZIRI MKUU,SOMA HAPO KUJUA
![]() |
| Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa |
RAIS Dk. John Magufuli leo amewasilisha bungeni jina
la Mbunge wa Ruangwa, Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya awamu ya
tano.
Spika wa Bunge, Job Ndugai
alipokea barua iliyotoka kwa Rais Magufuli kupitia kwa watumishi wa chombo
hicho cha kutunga sheria na baada ya kuifungua ndipo aliposoma ujumbe huo
uliotaja jina la Majaliwa ambaye alikuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu
Tawala za Mikoa na Serikali ya Mitaa (Tamisemi) anayeshughulikia elimu.
Baada
ya tangazo hilo ambalo lilipokelewa kwa shangwe na wabunge wengi, Spika Ndugai
aliahirisha bunge kwa dakika arobaini na tano kuwapa nafasi wabunge kutafakari
uteuzi huo kisha kumthibitisha bunge litakaporejea.
Waziri
Mkuu huyo mteule alizaliwa Disemba 22, 1960 na kupata elimu katika Shule ya
Msingi Mnacho kati ya mwaka 1970-1976 kabla ya kujiunga na shule ya sekondari
ya Kigonsera kati ya mwaka 1977- 1980.
Mwaka
1991-1993 alijiunga na Chuo Cha Ualimu Mtwara. Alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam mwaka 1994 na kuhitimu mwaka 1998 kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu cha
Stockholm nchini Sweden kwa masomo ya juu.
Amehudumu
katika nafasi mbalimbali tangu mwaka 1984 alipojiunga na utumishi wa umma kama
mwalimu mkoani Lindi, Katibu wa Chama cha Waalimu Wilaya, Katibu chama waalimu
Mkoa na Mkuu wa Wilaya.
Mwaka
2010 alichaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la Ruangwa mkoani Lindi kabla ya Rais
Mstaafu, Jakaya Kikwete kumteua mwaka 2012 kuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri
Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali ya Mitaa (Tamisemi) anayeshughulikia elimu.

No comments
Post a Comment