Zinazobamba

SAKATA LA KUWEPO VURUGU BUNGENI LEO,WANASHERIA WA LHRC WAMUANGUKIA SPIKA NDUGAI WASEMA AKIFANYA MCHEZO HUU ITAKULA KWAKE,SOMA HAPO KUJUA

Wabunge na wapambe wao wakiwa nje ya jengo la Bunge

NA KAROLI VINSENT
WANASHERIA kutoka kituo cha sheria na haki za Binadamu (LHRC) wamemtaka Spika wa Bunge Job Ndugai kutomhuruhusu kuingia Bungeni Dk Mohamed Shein na kutambulika kama Rais wa Zanzibar,
      Badala yake wamemtaka kumruhusu kuingia kama wageni wengine ili kuepuka vurugu.
     Akizungumza na kituo cha Redio cha Magic Fm katika kipindi cha Morning Magic,Mwanasheria wa (LHRC) Haron Sungusia amesema ni wakati wa Rais John Magufuli atakapolihutubia Bunge ni vema Spika wa Bunge akatumia busara ya kumtambulisha Dk Shein kama Mgeni rasmi kuliko Rais wa Zanzibar.
     “Namuomba Spika atumia busara ili aweze kuliokoa  Bunge kuingia kwenye fujo ni vema akamtambulisha Shein kama mgeni tu wa kawaida maana suala la Zanzibar sahivi lipo kwenye mgogoro mkubwa sana kutoka na uchaguzi kufutwa”amesema  Sungusia
        Sungusia ameongeza kuwa Kikatiba ukomo wa Dk Shein kwenye nafasi yake ya Urais kulishaishia tangu Novemba 2 mwaka huu ila  hoja inayotumiwa kuwa ukomo wa Urais wa Shein mpaka pale atakapohapishwa Rais mwengine haina mshiko kwa sasa kutoka na hali ya kisiasa ilivyo.
    Amebainisha kuwa hata sheria za Zanzibar bado zinaonyesha kutokuwa na uharali wowote wa Dk Shein kuwa Rais wa Zanziabr kutokana na Katiba kumbana.
    Kuibuka huko kwa Mwanasheria huyo kuzungumzia suala hilo,kuna kuja ikiwa ni teyari wabunge wanaounda UKAWA wametishia kutomruhusu Rais Magufuli kulihutubia Bunge bila suala la Zanzibarkutafutiwa ufumbuzi.
    Akizungumza na Fullhabari.blogs kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Juzi,Mwanasheria mkuu wa chama cha Demokrasia na Maendelea Chadema,Tundu Lissu amesema wao kama UKAWA hawatakubali kwa mazingira yeyote yale Rais Magufuli kulihutubia Bunge.

        Amesema kwa sasa watatumia Mbinu tofauti na ile waliotumia mwaka 2010 walipomgomea Rais mstaafu Jakaya Kikwete kwa kutoka nje ya Bunge ila sahivi wameapa kupambana ndani ya Bunge huku wakificha stairi watakayoitumia kwa kuwataka watanzania wasubiri waone.

No comments