Zinazobamba

JUKATA WAMTAKA MAGUFULI KUGEUKIA KATIBA MPYA..





Jukwa katiba nchini JUKATA limemtaka Rais mteule wa awamu ya tano wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh john Pombe Joseph magufuli kuendeleza mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya uliokuwa umesimama kutokana na shughuli za uchaguzi.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo Mwenyekiti wa jukwaa hilo Bw Deus Kibamba amesema kuwa mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya lazima uendelezwe kutokana na kwamba ndo ilikuwa agenda ya kitaifa kabla ya taifa halijaelekea kwenye uchaguzi.


Bw Kibamba amesema kuwa umuhimu wa kuwa na katiba ya kisasa umejizihilisha wakati wa uchaguzi mkuu ambapo mambo mengi yamekiukwa kutokana  kukosa katiba inayoeleza mambo katika misingi ya kuzingatia utawala bora.Aidha Bw Kibamba ameisihi 


Bwana Deus Kibamba amesema JUKATA wanamtaka Rais wa Tanzanaia Dr Magufuli baada ya kuzindua bunge na kupata mawaziri wake ahakikishe kuwa kwanza analitangazia Taifa Rasmi namna ya kurejea mchakato wa kupata katiba mpya,serikali ipeleke bungeni miswada ya mabadiliko ya serikali zinazosimamia mchakato wa katiba,kurejea makubaliano ya Dodoma ambayo yalitaka pia kupanua wigo wa wadau wahusika katika mchakato wa kupata katiba ikiwemo pia nyama vya wafanyakazi,ambapo amesema kuwa kama rais atafanya hayo anaweza kushinda mtihani wa serikali yake kuaminika na watanzania walio wengi.

Katika hatua nyingine jukwaa la katiba nchini Tanzania JUKATA wamemtaka Rais wa Tanzania Dr Magufuli aweze kuongoza jitihada za kuinusuru Zanzibar kutumbukia kwenye mkwamo au machafuko ya kisiasa hali ya sintofahamu iliyojitokeza baada ya uchaguzi ikiwa ni pamoja na kutambua kuwa hatua ya umoja wa serikali ya kitaifa iliyokuwa imeshafikiwa na wanzanzibar inapaswa kulindwa na kuheshimiwa.
Bwana KIBAMBA amesema kuwa kwa mujibu wa waangalizi wa JUKATA waliokuwa wakiangalia uchaguzi wa Zanzibar wameonyesha kuwa uchaguzi huo wa zanzibar ulifanyika na kumalizika kwa amani na hakukuwa na dosari kubwa zilizokuwa zinaweza kuwafanya uchaguzi huo kuahirishwa hivyo wameshangazwa sana hatua ya mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya Zanzibar Kufuta uchaguzi huo.

No comments