Zinazobamba

UKAWA WAMBULUZA KIKWETE NA NEC YAKE MAHAKAMANI,SOMA HAPO KUJUA



Leo tarehe  16 October 2015, Ukawa kupitia wakili wa CHADEMA,Peter Kibatala na mawakili wengine, wamefungua chini ya hati ya haraka sana (certificate of extreme urgency) shauri nambari 37 la mwaka 2015 katika Mahakama Kuu ya Tanzania (Main Registry) wakiomba Mahakama Kuu itoe tafsiri sahihi ya kifungu cha 104 (1) cha Sheria ya Uchaguzi Tanzania na itamke iwapo wapiga kura na watu wengine wenye shauku wanaruhusiwa au la kukaa KWA UTULIVU umbali unaozidi meter 200 kutoka kituo cha kupigia kura/kufanya majumuisho ya kura.
 
Pia wameiomba Mahakama Kuu itamke iwapo ni halali kwa Rais wa nchi kutoa matamko aliyoyatoa kwa namna ya katazo kwa wapiga kura/raia wenye shauku kukaa KWA UTULIVU umbali unaozidi mita 200 kutoka kituo cha kupigia kura/kufanya majumuisho.
 
Pia wameiomba Mahakama Kuu itamke iwapo Rais ana mamlaka hayo kisheria kwa kuzingatia Sheria ya Uchaguzi Tanzania.

Taarifa  hii  ni  kwa  mujibu  wa  Wakili  Peter  Kibatala  ambaye  ameshare  nasi  kwenye  ukurasa  wake  wa  facebook

1 comment

Anonymous said...

sawa sawa,mwanasheria.mwaka 2010 wapiga kura tulitakiwa,kama ilivyo sheria ya uchaguzi namba 104{1} tukisha maliza kupiga kura zetu,kwa walioona umuhimu,kukaa mita 200 toka mlango au chumba cha kupigia kura ili kuyasubiria matokeo yanayobandikwa mara bada ya zoezi la kuhesabu kura.mwaka huu ghafla,kinyume,kwa makusudi,tume imeikataa sheria ile lakini bila kuifuta.kibaya zaidi mkuu wa nchi mhe.jakaya kikwete kesha toa agizo la amri kwa polisi kutushughulikia raia yaani 'piga,shoot,kamata,vunja miguu'.mwaka 2010 hakukuwepo na UKAWA.sasa hivi nguvu,ari na umoja wetu umeongezeka mara alfu moja baada ya kuungana na kutuletea UKAWA .kulipeleka shauri hili mahakamani ndiyo njia pekee na sahihi katika kulinda haki zetu wapiga kura.yote kwa yote,iwe mvua,liwe jua chaguo letu ni mheshimiwa edward ngoyai lowassa.tumejiandaa kumpa kura zetu apite kwa ushindi mkubwa sana.