NI UCHAGUZI WA MISIBA TU,WATETEZI WA WANYONGE WANAZIDI AGA DUNIA,SOMA HAPO KUJUA

ALIYEKUWA mbunge
wa jimbo la Ludewa ambaye anatetea kiti hicho katika uchaguzi wa Oktoba 25, Deo
Filikunjombe amefariki dunia katika ajali ya helikopta. Anaandika Faki Sosi …
(endelea).
Pia Kapteni William Silaa, aliyekuwa akirusha
helikopta hiyo, ikitokea uwanja wa Dar es Salaam kwenda jimboni Ludewa, mkoani
Iringa, pamoja na mdogo wa Filikunjombe, aitwaye Haule, pia wamefariki dunia
katika ajali hiyo.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya
habari, Filikunjombe alikuwa katika msafara wa kwenda jimboni kwake kukamilisha
ngwe ya mwisho ya kampeni.
Taarifa za mapema
za ajali hiyo zimetangazwa na Jerry Silaa, ambaye ni mtoto wa Kapteni Silaa
aliyefariki dunia katika ajali hiyo. Silaa aliandika katika akaunti yake ya
mtandao wa picha, Instagram, akisema ajali
imemhusisha baba yake ambaye ni rubani.
Taarifa za ajali
hiyo zilianza kuenea tangu jioni jana lakini mpaka mchana alasiri hii, Jeshi la
Polisi limeshindwa kutoa taarifa rasmi inayoonesha majina yote ya waliokuwa
kwenye helikopta hiyo wala kutaja kampuni inayoimiliki.
Kituo cha
televisheni cha ITV kiliwasiliana kwa simu na Mkuu wa Operesheni wa Jeshi la
Polisi nchini, Paul Chagonja, akimuuliza undani wa tukio hilo lakini ameshindwa
kujibu hoja hizo.
Angalau Kamishna
Chagonja alisema helikopta hiyo ilianguka usiku wa kuamkia leo eneo la Pori la
Hifadhi ya Selous, ukanda wa Rufiji mkoani Pwani.
“Mtu aliyeiona ametoa taarifa kuwa ilianguka lakini
hatujafanikiwa kupata uhakika wa taarifa kuwa iliungua ilipofika chini…
helikopta imesajiliwa kwa Na. 5Y-DKK,” alikaririwa akisema Kamishna Chagonja.
Silaa ambaye
baba yake amekufa katika ajali hiyo alichapisha taarifa ya kuarifu tukio hilo
akisema, “nimepokea taarifa kutoka kwa timu ya uokoaji kuwa abiria wote
waliokuwa kwenye helikopta hiyo wamefariki dunia akiwemo Baba yangu mzazi na
rafiki yangu Deo Filikunjombe.”
Kwa kawaida, hakuna ndege inayoondoka uwanjani, hata iwe ndogo
kiasi gani, lazima inakuwa na orodha ya watu waliosafiri (manifesto). Wala hakuna
kitu kama haijulikani mmiliki wake.
Ajali hiyo inasababisha kukata roho kwa mgombea wa sita wa
ubunge baada ya Dk. Emmanuel Makaidi wa National League for Democracy (NLD),
aliyekuwa akigombea jimbo la Masasi mkoani Mtwara, kufariki jana mchana baada
ya kuugua ghafla nyumbani kwake Masasi mjini.
Filikunjombe
alikuwa mbunge kutoka Oktoba 2010. Kabla ya Dk. Makaidi, walioaga dunia na
majimbo yao kwenye mabano ni Dk. Abdallah Kigoda (Handeni mjini, CCM), Estomii
Mallah (Arusha mjini, ACT-Wazalendo), Celina Kombani (Ulanga Mashariki, CCM) na
Mohamed Mtoi (Lushoto, Chadema).
Uchaguzi wa majimbo hayo umeahirishwa katika majimbo hayo hadi
mwezi ujao.
Habari hii kwahisani ya Mwanahalisi oline
No comments
Post a Comment