Zinazobamba

NAFASI YA UWAZIRI MKUU YAIPASUA KAMBI YA MAGUFULI,JANUARY MAKAMBA NA MWIGULU WAJIAPIZA,SOMA HAPO KUJUA

NAFASI ya Uwaziri mkuu endapo Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM,john Magufuli akiwafanikiwa kuwa Rais wa awamu ya tano,imetajwa kukigawa chama hicho makundi mawili.(Mtandao huu umedokezwa),Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
      Taarifa za kuaminika ambazo mtandao huu umezipata kutoka ndani ya Kamati ya ushindi ya CCM,zinasema kumeibuka makundi mawili yanayopambana kufa na kupona kuhakikisha wanateuliwa kushika nafasi hiyo kubwa  Serikalini,
      Chanzo chetu hicho  kinasema makundi mawili hayo ni moja likiongozwa na January Makamba pamoja na Kundi jengine linaloongozwa na Mwigulu Nchemba ambao wote kwa pamoja wanajiapiza kuteuliwa nafasi ya Uwaziri mkuu.
      “Ujue sahivi hawa mabwana (January na Mwigulu) wamekigawa chama ndugu,leo wanajiona kama wao ndio wenye chama,wanajiapiza kuwa lazima washike nafasi ya uwaziri mkuu,yaani wamekuwa na kiburi cha ajabu mpaka tunashangaa”amesema chanzo chetu hicho.
      Kuibuka kwa taarifa hizi kunakuja ikiwa imebaki siku nane kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika hapo octoba 25,kwa mujibu wa marafiki wa Karibu wa Januray Makamba ambaye ni msemaji wa Kamati ya Ushindi,wamesema ni kwamba Makamba ameshajihakikishia asilimia 100 kuwa yeye ni waziri mkuu kwenye Serikali ya Magufuli.
    “Sikufichi hizi taarifa ni za kweli maana January Makamba amekuwa akijihamini kwamba lazima awe waziri mkuu,bira hata sisi kutuambia sababu ya yeye kujiamini huku ikizingatia hata kabla ya uchaguzi mkuu,kufanyika bado,”

      Mbali na Makamba na Mwigulu,makada wengine  wa CCM wanaojiapiza lazima washike nafasi hiyo ni Wiliam Lukuvi,pamoja na Dk Mwakyembe ambao wote inatajwa pia wanainyemelea nasafi hiyo.

No comments