SERIKALI YAMTOA MKURUGENZI WA MWANZA,KISA KAGOMEA BAO LA MKONO,SOMA HAPO KUJUA
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman KInana akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo |
MKURUGENZI wa
Jiji la Mwanza, Hassan Hida, anadaiwa kuhamishwa katika jiji hilo kwa kile
kinachodaiwa ni kukataa kucheza ‘bao la mkono’ katika Jimbo la Nyamagana. Anaandika Moses Mseti, Mwanza … (endelea).
Inadaiwa kuwa mkurugenzi huyo ameondolewa
katika jiji hilo baada ya kukataa kucheza ‘bao la mkono’, huku akituhumiwa
kumuunga mkono Mgombea Urais wa Chadema, Edward Lowassa anayeungwa mkono na
Muungano wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Inaelezwa kuwa
Hida kabla ya kuondolewa katika nafasi hiyo na kupewa kazi nyingine serikalini,
baadhi ya viongozi wakubwa wa mkoa huo, waliitisha vikao vya kumlazimisha
kucheza ‘bao la mkono’ jambo ambalo alipingana nalo na kibarua chake kuota
mbawa.
Hata hivyo baada
ya mkurugenzi huyo kukataa mchezo huo hatari, viongozi hao wa juu walianza
kuwasiliana na viongozi wa kitaifa wakiomba kuondolewa kwake jambo ambalo
halikuchukua muda mrefu na kuhamishwa.
Mtoa taarifa hizi
amesema kuwa mkurugenzi huyo, aliondolewa kutokana na kuwagomea viongozi hao
wanaodaiwa kuunda mbinu chafu za kulazimisha ushindi katika Jimbo hilo la
Nyamagana ambalo historia ya wabunge waliowahi kuongoza wamekaa kwa awamu moja.
Mtoa taarifa
aliendelea kudai kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kimejipanga kulazimisha ushindi
wowote ule hata kama ni wa kumwaga damu lakini washinde jimbo hilo kitendo
ambacho kitasababisha uvunjifu wa amani.
“CCM wameisha
jiapiza kwamba jimbo hili na lile la Ilemela ni lazima washinde hata kama ni wa
kumwaga damu na huyu mkurugenzi kahamishwa kwa sababu aliwakatalia kutangaza
matokeo ya uongo,” amesema mtoa taarifa huyo.
Hata hivyo Hida ambaye alishawahi kuwa Mkurugenzi wa Jiji la
Arusha, kabla ya Mwanza na kuhamishwa katika nafasi hiyo, inadaiwa kuwa na
msuguano na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo, ambao wote walihamishiwa
Mwanza kutoka Arusha.
Hata hivyo Hida alipotafutwa na gazeti hili kuzungumzia tuhuma
za kuondolewa kwake jijini hapa zinazohusishwa na siasa, simu yake ya mkononi
haikupatikana.
Jimbo la Nyamagana linashindaniwa na Ezekia Wenje (Chadema),
anaetetea nafasi hiyo, Stanslaus Mabula (CCM) na wagombea wengine wa ACT, TLP.
Habari hii kwahisani ya mwanahalisi oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni