MASIKINI WAFANYAKAZI WA UCHUMI SUPERMARKET,SASA WAIANGUKIA SERIKALI WALIZWA MABILIONI,SOMA HAPO KUJUA
WASAMBAZAJI
bidhaa za kampuni mbalimbali zilizokuwa zikifanya kazi na kampuni ya Uchumi
Supermarket ya Uchumi wameitaka Serikali kuwasaidia kulipwa madeni wanayoidai
kampuni hiyo baada ya kufungwa bila ya kupewa taarifa yanayofikia bil. 4.4. Anaandika Hamisi Mguta … (endelea).
Kufungwa
kwa kampuni hiyo ambayo chimbuko lake ni nchini Kenya kunadaiwa kuwa kunatokana
nakufilisika hali iliyopelekea kushindwa kulipa madeni ya wasambazaji hao
wakubwa na wadogo.
Wakizungumza na
MwanaHALISI Online kwa nyakati tofauti baadhi ya wasambazaji hao ambayo idadi
yao 202, wamesema serikali ndio chombo pekee cha kuwasaidia ili kupata haki zao
kwani hata wakikaa na ubarozi wa Kenya ambako ndiko kampuni hiyo inatokea,
hawataweza kufanya kitu bila ushirikiano wa Serikali.
Mwenyekiti wa muda wa madai ya wasambazaji
hao, Joseph Mlay amesema kufungwa kwa Supermarket hiyo bila taarifa hakujaleta
picha nzuri ya kibiashara kutokana na hasara iliyosababishwa na tukio hilo.
Mlay ambaye
anafanya kazi ya usambazaji wa mabarafu katika Supermarket hiyo amesema tayari
hatua za awali zimechukuliwa ikiwa ni pamoja na kuandika barua kwa Mkuu wa mkoa
wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick na Meya wa jiji Didas Masabuli kuwataka
kuongeza nguvu ya kutatua tatizo hili kwani wakati wa ufunguzi wakampuni hiyo
walikuwepo.
Katibu wa wasambazaji hao ambaye pia ni akaunti meneja wa
kampuni ya Chai Bora, Floriana John amesema kampuni yao inaidai Uchumi
Supermarket mil. 37 katika kipindi cha miezi miwili ambazo zimepelekea
kumeporomoka kwa uchumi na maendeleo yao na uaminifu kwa wateja waliokuwa
wakishirikiana nao kutokana na madeni wanayodaiwa.
John amesema katika tukio hilo wengi walioathirika ni
wajasiriamali wadogo wanaofanya biashara za mboga mboga kutokana na ugumu
mkubwa wanaoupata katika kuandaa biashara zao kutoka mashambani huku kipato
chao kikiwa kidogo zaidi.
Naye Msambazaji wa bidhaa za kampuni ya Bidco Oil & Soap
ambayo pia inadai Mil. 10 kwa zaidi ya miezi sita sasa, Baraka Sawe amesema
madhara makubwa yameikumba kampuni hiyo ikiwa ni pamoja na kukosa soko kutokana
na kutegemea soko katika Supermarket ya Uchumi hivyo kupelekea kushindwa
kuendesha biashara.
Kwahisani ya
mwanahalisi oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni