MAHAKAMA KUU PACHIMBIKA TENA,WAKILI KIBATALA AIENYESHA SERIKALI,SASA MAHAKAMA KUAMUA KESHO MITA 200,SOMA HAPO KUJUA
NA
KAROLI VINSENT
ZIKIWA
zimesalia siku tatu kuelekea Uchaguzi Mkuu, Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya
Dar es Salaam, kesho inatarajia kutoa uhamuzi katika kesi ya kikatiba kuhusu
umbali wa mita 200 wanaotakiwa kukaa wapigakura baada ya kupiga kura.
Katika
kesi hiyo namba 37/2015 iliyofunguliwa na mpigakura Amy Kibatala, ilianza
kuunguruma mahakamani hapo tangu mwanzoni mwa wiki chini ya Jopo la Majaji
watatu.
Wakati
uhamuzi huo ukisubiliwa kwa hamu kesho,ambapo jana Mahakama iliahirisha kesi
hiyo kutokana na mvutano wa kisheria baina ya pande mbili kati ya mlalamikaji
aliyewakilishwa na Wakili Peter Kibatala, huku upande wa Serikali, ukiwa na
wanasheria nane, wakiongozwa na Mwanasheria Tulia Akson.
Katika
mvutano huo, ulioanza saa 3:17 asubuhi na kufikia tamati saa 11 jioni, Wakili
Kibatala aliiomba mahakama iangalie maana ya kifungu cha 104 katika haki ya
wapigakura kukaa kwa utulivu umbali wa mita 200 pamoja na kutoa tamko kwa
wapigakura na watu wenye shauku kwamba wana haki ya kukaa umbali huo kwa utulivu.
“Majaji
msingi wa shauri hili ni kuwa mara kadhaa NEC (Tume ya Taifa ya Uchaguzi)
imekuwa ikitoa tamko kwamba wapigakura na watu wenye shauku ya kufuatilia
mwenendo wa matokeo wasikae popote baada ya mchakato huo, ambapo inadaiwa
katazo hilo limetoka kwenye kifungu cha 104,”alieleza Kibatala.
Kwa
upande wa Serikila, Mwanasheria Akson alidai kuwa shauri hilo litupiliwe mbali
na mahakama, kwani NEC haikuvunja sheria kwa kutoa agizo hilo la umbali wa mita
200.
Kutokana
na mvutano huo, Jopo hilo la majaji likiongozwa na Mwenyekiti Jaji Sakieti
Kihiyo liliahirisha kesi hiyo hadi jana ili itolewe maelezo maalum.
Hata
hivyo, shahuku ya Wanasheria kutoka pande zote mbili na watu mbalimbali
waliofika mahakamani hapo jana kufatilia kesi hiyo, ilikatika baada ya Jaji
Kihiyo kusema kwamba uhamuzi utatolewa kesho.
Jaji
Kihiyo alisema wakati wanaahirisha shauri hilo jana, walisisitiza kwamba kesi
hiyo ingetajwa jana kwa ajili ya kutolewa maelezo maalum, hivyo maelezo hayo ni
uahamuzi utakaotolewa kesho.
“Leo
tulisema kwamba tutatoa maelezo maalum, kuhusu kesi hii… hivyo maelezo hayo ni
kwamba tukutane kesho saa nne asubuhi kwa ajili ya kutoa uhamuzi,”alisema Jaji
Kihiyo.
Mara
baada ya jopo hilo kutoka katika chumba cha mahakama, ilisikika minong’ono baadhi
ya watu wakidai kwamba hakuwatarajia kusikia hivyo.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni