MKE WA MCHUNGAJI MTIKILA AJICHANGANYA KUHUSU CHANZO CHA KIFO CHA MUMEWE,AWARUKA RAIS KAGAME NA OTHUMAN WA TISS,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni Mke wa Mchungaji christofa Mtikila ,be Georgia Mtikila akizungumza na waandishi wa Habari leo kuhusu chanzo kifo cha mumewe |
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida Mjane wa mchungaji
Christofa Mtikila amejichanganya mwenyewe kuhusu chanzo cha kifo cha mumewe
.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Hayo yamegundulika
leo wakati wa mkutano na waandishi wa habari ulioandaliwa na Familiya ya
Mtikila kuzungumia kifo hicho, ambapo Be
Georgia Mtikila ambaye ni Mke wa Mtikila.
amesema anahuhakika
chanzo cha kifo cha mumewe ambaye alikuwa mwenyekiti wa chama cha DP kimepangwa
na Mgombea wa Urais kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema-
Ambaye
anaungwa mkono na UKAWA Edward lowassa pamoja na Waziri mkuu mstaafu Fredrick
Sumaye kwa madai kuwa Marehemu Mtikila alipokuwa akifanya mahojiani kwenye
kituo cha StarTv aliwatuhumu viongozi
hao kuhusika na kashfa mbali mbali.
Mama Mtikila amesema mara baada ya kipindi
hicho kumaliza amedai kuwa mumewe alipigiwa simu na watu mbali mbali
wakijitambulisha kuwa wametumwa na Lowassa na Sumaye kwa kutaka kumpa nusu
bilioni ili amchafue Mgombea wa Chama cha Mapinduzi CCM John Magufuli , Amedai
mara mumewe huyo kukataa ndio vitisho mbali mbali vikatokea,
MPANGO WA
KUMUUA MTIKILA
Mjane huyo amefichua mpango anaodai ni wa kumuua
Mchungaji mtikila, amedai mumewe
alitafutiwa gari na Victoria Manyahi ambayo amema madereva hao hawakuwajua wala kuwaona na hata
makubaliano ya kulipa hayajui
Amesema
licha ya madereva hao kutowajua, jambo ambalo linampa shida ni Mlinzi wa
kujitolea aliyekuwa anamlinda mtikila (body guard) mgaya Patrick ameadia hajamuona usoni kwake kabla ya na
hata baada ya kifo cha mumewe.
“Pamoja na
juhudi zangu zote za kumpigia simu mara
kadhaa aje anijuze chanzo cha kifo cha meme wangu sijampata ndio maana napata
tabu sana juu ya kifo hichi”amesema
Hata hivyo mjane huyo amesema hana imani na
ripoti iliyotolewa na Jeshi la Polisi kuhusu kifo cha Mumewe amemuomba Rais
Jakaya Kikwete kuunda tumehuru kuchunguza ajali hiyo.
KUJIKANYAGA KUHUSU KIFO CHA MTIKILA,
Katika
hali ya kushangaza mjane huyo
ametofautiana na mumewe kuhusu namna
alivyokuwa anatishiwa maisha,
Kwani mara
kadha marehemu mtikila alikuwa anamtuhumu Rais wa Rwanda Paul Kagame akidai
kuwa anashirikiana na Mkurugenzi wa
Idara ya Usalama wa Taifa, Rashid Othman kutaka kumuua,
Akizungumza
na waandishi habari kwenye ukumbi wa idara ya habari maelezo miezi miwili iliyopita kabla ya mauti ,Marehemu Mtikila
alisema Kagame amekuwa akimwinda mara kwa mara tena akimtumia bosi wa usalama
wa Taifa kutaka kumuua,
Alipuulizwa
na waandishi wa habari,mjane wa Mtikila kuhusu shutuma za marehemu mtikila kipindi
yupo hai kwamba Usalama wa Taifa pamoja na Rais Kagame kutaka kumuua,iweje leo
waibuke wamtaje Lowassa na kumruka Kagame na Othuman ambapo mara kwa mara
marehemu alikuwa anawatuhumu walikuwa wanataka kumuua,
Akajibu kwa kumuomba Rais Kikwete aunde tume ya
kumchunguza jambo hili,
Maoni 1
huyu mama akamatwe na polisi kwa uzushi na wehu wa kuweweseka.anapolikaqtaa jeshi la polisi hajui hyo ndiyo dola endelevu.kikwete amebakiza siku nne akabidhi mamlaka ya nchi kwa rais mpya lakini huyu mama hajui hata kama kuna uchaguzi mkuu tanzania.ana matatizo makubwa.
Chapisha Maoni