SERIKALI YAVIANGUKIA VYOMBO VYA HABARI,NI KUHUSU UCHAGUZI MKUU,SOMA HAPO KUJUA
WAKATI zikiwa zimebaki siku tatu kabla ya siku ya
kupiga kura kufika hapo jumapili ya wiki hii,Serikali imevitaka vyombo vya
habari kuripoti habari zenye usawa na haki ili kuliepusha Taifa kuingia katika
uvunjifu wa amani.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo,
Rai
hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo,Assah
Mwambene wakati wa mkutano na waandishi wa habari, wenye lengo la kutoa tasmini fupi kulekea uchaguzi mkuu
ambapo amesema wanahabari wanajukumu kubwa la kulida amani ya Tanzania kwa
kuhakisha wanaripoti taarifa zisozokuwa na upelendeleo ,
Amesema
machafuko mengi yaliyokokea katika nchi za Rwanda,Kenya vyombo vya habari
vimehusika kwa kiasi kikubwa kutokana
kuripoti taarifa zenye chuki na zilizojaa
upotoshaji huku akiwatadhahalisha waandishi wa Tanzania kujiepuka na hatari
hiyo,
Amesema
vyombo vya habari vinatakiwa kujiepuka na michezo ya wanasiasa ambao wenye
malengo ya kuvuruga amani huku akitolea mfano lugha zinazotolewa na Magazeti
kama maneno ya “Gharika” “Tsunami” “Gori la mkono” amedai maneno haya yanaweza
kuchangia kuvuruga amani ya nchi.
Hata
Hivyo,Mwambene ambaye pia ni msemaji wa serikali amewaomba Watanzania kutoviamini
vyombo vya habari katika uchaguzi huu.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni