KIKWETE AWAPA VYEO WATUHUMIWA WA UFISADI,NI DAKIKA ZA LALA SALAMA ZA MADARAKA YAKE,SOMA HAPO KUJUA
WAKATI akiwa amebakiza saa 24 tu ili Rais
Jakaya Kikwete aachie madaraka ya Urais aliyokuwa nayo,katika hali ya
kushangaza Rais Kikwete amewapa vyeo,watuhumiwa waUfisadi katika nafasi mbali
mbali.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Kwa mujibu
wa taarifa iliyotolewa na Ikulu kwa vyombo vya habari inaonyesha Rais Kikwete kufanya uteuzi kwenye
nafasi mbali mbli ikiwemo nafasi za Ukatibu mkuu wa Wizara pamoja na nafasi za
Afisa tawala za mikoa.
Katika Uteuzi huo alioufanya kwaanzia siku ya jana
usiku Rais Kikwete amemteua aliyewai
kuwa Katibu wa Wizara ya nisharti na madini, Ndugu Eliakim Maswi kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara,
Awali Maswi
alituhumiwa na Bunge na nne katika kashfa ya ukwapuaji wa mabilioni ya shilingi
kwenye iliyokuwa Akount ya Tegetea Escrow pale Benk kuu ya Tanzania B.O.T.
Kwa mujibu wa
mapendekezo ya zaidi ya tisa ya Bunge kuhusu watuhumiwa wa ufisadi wa Escrow
jina la Maswi lilitajwa na bunge kwa kumuuomba Rais Kikwete amuondoe kwenye
nafasi ya Ukatibu mkuu hapo wizara ya nisharti na madini jambo mbalo kikwete
alilitekeleza ila la kushangaza leo tena amemteua kwenye nafasi nyingine,
Sanjari na Maswi pia Rais Kikwete
amemutea aliyekuwa mkurugenzi wa mamlaka ya Bandari nchini TPA, Mhandisi Madeni
Kipande ambaye anakuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi.
Kipande ambaye aliondolewa nafasi yake ya
ukurugenzi bandarini baada ya Waziri wa uchukuzi Samwel Sitta kuunda tume ya
kumchunguza mkurugenzi huyo,ambapo baada ya tume hiyo kumaliza kazi yake ndio
ikamfanya Sitta kumwondosha Kipande bandarini hapo kutokana na kashfa mbali
mbali zilizorudisha nyuma Bandari hiyo.
Hata hivyo Kipande
aliwai tuhumiwa na vyombo vya habari kwa kufanya vitendo vya unyama na ufisadi
bandarini hapo kwa mujibu wa chanzo chetu kilichokuwa kinamfuatilia kipande
kilionyesha ufisadi wake wa kutisha kama ifuatavyo.
chanzo hicho kilizidi
kusema Kipande amekuwa
akijivunia kwa Wanyakazi wake hapo
Bandarini kwamba anaweza kufanya lolote na hakuna wakumzuia,ambapo amesimamisha
watu kazi zaidi ya miaka miwili huku wakiwa wakipokea mishahara pamoja na
malupulupu huku wakiwa nyumbani bila hata ya kufanya kazi.
Chanzo
hicho kiliwataja wafanya kazi hao,miongoni mwao ni Mama Muhindi,ambaye alikuwa
Mkurugenzi wa Masoko TPA,ambaye alisimamishwa kazi na Kipande kwa Madai alikuwa
anavujisha siri(madudu)za TPA kuhusu kwenye vyombo vya
Habari,licha ya mkurugenzi kipande alishindwa kutokea wala kukanusha kwenye
vyombo vya Habari juu ya Ufisadi huo ,
Tuhuma,zinginene
zinazozidi kumkabili kipande kuhatarisha usalama wa Bandarini kwa kutokuna na
kutokuwepo na Kamera CCTV pamoja na mita za kupima mafuta yanayoingia nchini
kutokafanya kazi kwa miaka mitatu sasa.
Jambo la kushangaza Mama huyo Muhindi,alisimaishwa kazi tangu agosti 2013 na
kipande,lakini hajahojiwa wala
kurudishwa kazini ,huku akizidi kuendelea kuchukua mshahara na Marupumarupu
mengine bila kufanya kazi hadi sasa wala hajahojiwa na mamlaka yeyote.
Chanzo,hicho kilizidi kutaja orodha ya Wafanyakazi walionewa na Kipande ambae ni Mfanyakazi mwingine ndugu Msemo,aliyekuwa Afisa
Ununuzi,naye alisimamishwa kazi tangu agosti2013 kwa tuhuma zisizokuwa za
Ukweli wowote, lakini mpaka sasa naye anaendelea kuchukua mshahara pamoja na
marupurupu yote pasipo kufanya kazi.
Waliosimamishwa na kipande kwa tuhuma hewa
Hery Arika,aliyekuwa
Men eja Biashara wa Bandari ya Dar es Salaam,alihamishiwa makao makuu na
kuambiwa kuripoti idara ya utawala tangu April 2013 huku akiendelea kulipwa mishahara na
marupurupu yake bila kufanya kazi kwa mwaka mmoja sasa,kwa madai ya Kipande
hamtaki.
Ajira za Upendeleo,
Kama kuna mgogoro
unaofuka Moshi Ndani ya Bandari basi ni huu unaotokana na Ajira za Mhandisi Alois Matei,ambaye ni Naibu
Mkurugenzi mkuu(Maendeleo ya Miundombinu)na mhandisi William Shilla,ambaye ni
mkurugezni wa Uhandisi.Taharifa zilizopo zinasema kuwa Wahandisi hawa wawili
waliajiriwa na Kipande kupitia
Mlango wa Nyuma ,pasipo kufuata taratibu za sheria.
Huu ni Mwenderezo wa
Unyama unaofanywa na Kipande ndani ya Bandari pasipo kuchukuliwa Hatua yeyote
kutoka kwenye Taasisi za Kupambana na Rushwa TAKUKURU,wala Wizara husika ya
Uchukuzi ambao,mamlaka hiyo iko chini yake.
Huku,Kipande
akinijinadi kwenye mkutano na Uongozi wa mamlaka hiyo,akisema mtu yeyote
atakaye pingana nae anamngoa kwani yeye na mamlaka hiyo ya Bandari hawapati
hasara yeyote bali serikali ndio inapata hasara,na kama yuko mtu yeyeto atakaye
pingana naye(Kipande )basi atamfukuza Kazi.
Duru, hizo zinasema mzee Kipande amekuwa akifanya Vitendo hivyo vya Kifisadi
huku akijinadi Hakuna mtu wa kumng”oa nafasi hiyo kwa Madai,eti anajuana Kigogo
mmoja aliyoko Ikuru ya Jakaya
Kikwete,ambae amekuwa karibu na Kipande.Ndio maana Amekuwa akifanya Vitendo
hivyo akijua hakuna mtu wakumchukulia Hatua zozote
Hakuna maoni
Chapisha Maoni