Zinazobamba

HIVI NDIVYO MWAKYEMBE ALIVYOJIMALIZA MWENYEWE KWENYE SAKATA LA RICHMOUND,UONGO WAKE WABAINIKA,SOMA HAPO KUJUA

WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Harrison Mwakyembe

Huyo ni Mwanasheria Mwakyembe alivyowahadaa umma.
Nasema hivyo kwasababu Kisheria, Kamati teule ya Bunge huteuliwa na Spika wa Bunge kwa suala maalum na baada ya kumaliza suala husika na kukabidhi ripoti Kamati hiyo huvunjwa. Hii si sawa na Kamati za kudumu za Bunge. Hivyo basi baada ya Ripoti ya Richmond kujadiliwa Bungeni na kutolewa maazimio ya Bunge, na hatimaye Samwel Sitta kuufunga mjadala(baada tu ya lengo la kumtoa Lowassa kutimia) Mwakyembe na Kamati yake waliishia hapo (soon thereafter akapewa Uwaziri).
Huyu msaka tonge mwakyembe, alitamka Bungeni (na Hansard ipo) kuwa " Kuna mambo waliamua kuyaacha ili kuiokoa serikali ya Jk na ccm isianguke"
SASA MASWALI YANGU NI HAYA YAFUATAYO MWAMBIENI AJIBU:
1. Kwanini walitumia pesa ya Wananchi, wakasafiri hadi Texas Marekani kuhoji watu lakini hawakumhoji Lowassa aliyekuwepo Dar Es Salaam.
2. Ni kwanini watumie pesa ya Wananchi halafu aje atwambie eti "Kuna mambo wameyaacha kuinusuru serikali isianguke"..
3. Alikuwa anamnusuru nani? Maana Waziri mkuu aling'atuka na Baraza la Mawaziri likavunjika. Aeleze alimnusuru nani asianguke?!
4. Aeleze ni kwanini amekaa kimya miaka 8 ndo aje kutwambia hizo pumba muda huu?! Alikuwa wapi?
5. Anatwambia sisi wananchi muda huu ili tufanyeje!? Kwani sisi ni Polisi au Mahakama?
6. Lowassa yupo Tanzania na hana kinga ya kutoshitakiwa, kwanini mpaka leo hawajamkamata kama Yona na Mramba?!
7. Mwakyembe anajua 'rules of natural justice'?! Kwanini hawakumpa nafasi ya kumsikiliza Lowassa kabla ya kwenda kumhukumu Bungeni!?
8. Kwanini Mwakwembe asiongelee pia Escrow, Epa, Twiga kupanda ndege, Kiwila Coal Mine, Rada na nyinginezo?! Ufisadi ni Richmond tuu!?
9. Wakati Lowassa anabeba Richmond, baraza la Mawaziri na Mwenyekiti wake walikuwa wapi?! Mwanasheria Mkuu wa Serikali je?
Mwakyembe ni mnafiki na Muongo, na kwa kazi hiyo anapata mkate wake.

 TAZAMA VIDEO YA MWANDISHI KUBENEA ALIVYOMJIVU MWAKYEMBE NA SLAA KUHUSU RICHMOUND 



Hakuna maoni