Zinazobamba

NI WIZI NI WIZI WA KURA KILA KONA,MAKARATASI YA KURA YAKAMATWA ,HAKIKA YA GORI LA MKONO YATIMIA,SOMA HAPO KUJUA


Hii  imeripotiwa  kutokea  Moshi


Hii  imeripotiwa  kutokea  Pemba


UCHAGUZI mkuu ni kama umehariba ndivyo naweza kusema baada ya maeneo mengi nchini kukamatwa kwa kura feki mbazo teyari zikiwa zimewekwa alama ya vema kwa wagombea wa Urais,Ubunge na udiwani kwa wagombea wa chama cha Mapinduzi CCM.
       Taarifa kutoka kwenye vituo mbali mbali ambazo Fullhabari,blogs imezipata zinasema shehena ya katasi za kupigia kura zikiwa zimakamatwa kwenye maeneo mbali mbali.
       Tukio ambalo limewashangaza wengi ni lile lilotokea mkoani Bukoba ambapo karatasi kibao zikiwa zimekamatwa kwenye chumba cha wanafunzi wa kidato cha sita,zikiwa zimeshawekwa alama ya vema kwa wagombea wa ngazi zote wa chama cha Mapinduzi CCM,
       Akithibitisha kukamatwa kwa kura hizo feki,Mkurugenzi wa ulinzi wa chama cha Demokrasia na maendeleo chadema  Bwan Lwakatare amekiambia kituo cha Televisheni cha Itv akisema kura hizo zimekamatwa kutokana na juhudu kubwa kati ya wananchi pamoja na jitihada za chama hicho.
        Amesema Rais Jakaya Kikwete anatumia madaraka yake vibaya kutaka kuvuruga uchaguzi mkuu,kwa kuhusika au kunyamazia wizi wa kura sehemu mbali mbali kwa kujenga chama chake,
     KARA ZENGINE FEKI ZAKAMTWA PEMBA NA MOSHO,
Sanjari na Bukoba pia shehena ya kura nyingine feki zimekamatwa mkoani Kilimanjaro pamoja na kisiwa cha Pemba zikiwa zimewekwa alama ya vema kwa wagombea wa CCM kwa ngazi zote,

      Kwa mujibu wa mtoa taarifa wetu aliyoka sehemu hizo amesema kura hizo zimekatwa kwenye magari mbali aina ya daladala pamoja na hari ndogo aina ya vitala zikiwa teyari zimembeba mgombea wa Urais kupitia CCM,John Magufuli
      VUNJU KURA FEKI ZANASWA KWA WASIMAMIZI WA KITUO,

          Wizi huo wa kura umetokea tena huku jimbo la Vunjo baada ya wasimamizi wa uchaguzi kukamatwa na kura feki zinazokibeba chama cha Mapinduzi CCM kwenye wagombea wake wote kama unavyotizama picha hizo,

   SUMBAWANGA PIA WIZI WANASWA,
Watu wapatao 200 wameteketeza  kwa moto vifaa vya kupiga kura  huku wengine wakiwajeruhi wasimamizi wa uchaguzi kwa kile kinachoonekana kuwa ni hofu ya kusambazwa kwa kura feki.

Katika tukio lililotokea wilaya ya Sumbawanga, watu hao wanadaiwa kuteketeza vifaa mbalimbali yakiwamo makasha  45 ya kuhifadhia   kura  wakidai kuwa yalikuwa na kura ambazo  tayari  zilikuwa  zimeshapigwa .

Akizungumza na mwandishi wa habari  hizi kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa , Jacob Mwaruanda  amethibitisha kutokea  kwa tukio  huo  katika  kijiji  cha Zimba , Bonde la Ziwa Rukwa  wilayani Sumbawanga .

“Niko  njiani  nikielekea  katika eneo  la tukio  ni kweli  limetokea  usiku wa kuamkia leo  ….. vifaa hivyo  vilikuwa  vikisafirishwa  kwenda tarafa ya Milepa Bonde la Ziwa Rukwa  “ alisema

Akisimulia tukio hilo, Kamanda Mwaruanda alidai kuwa watu wapatao 200 wakiwa na silaha za jadi yakiwemo  mapanga , marungu , mawe na  mikuki waliweka vizuizi  vya  mawe makubwa  barabara  kijijini Zimba  na kulizuia  gari  lililokuwa likisafirisha  vifaa  hivyo  vya kupiga kura  kwenda Tarafa ya Milepa.

Alieleza kuwa  gari hilo lenye  namba za usajiri T 865 BEU  likiwa na maofisa  wawili  wasaidizi wa uchaguzi  na dereva  lilizuiliwa na  watu hao  wenye hasira  na kuchoma  vifaa  vyote  vya  kupigia  kura  ambapo  watu wanane  wanashikiliwa na Jeshi la Polisi .

Kwa mujibu wa Mwaruanda  hakuna mtu yeyote  waliokuwa wakisafiri katika  gari hilo  aliyereruhiwa  katika tukio hilo ambao  majina yao  hayakuweza kufahamika mara moja  .

Kwa upande wake, Msimamizi wa Uchaguzi  wa Wilaya  ya Sumbawanga , Adam Missana  akizungumza na  mwandishi wa habari  hizi  kwa njia  ya simu  amekiri  kutokea kwa tukio hilo huo  akidai ulitokea  katika kijiji cha Zimba  kati ya saa tatu na nne  usiku wa kuamkia leo .

KASORO LUKUKI
Licha wizi huo kutokea kwenye karibia maeneo yote nchini,pia kumetokea kasoro lukuki huku maeneo mengi mpaka kufikisa saa tisa jioni watu walikuwa hawajapiga kura kutokana na karatasi za kura kuisha kwenye vituo.
Hayo yamegundulika katika vituo vya Jimbo la Kibamba liloko jijini Dar es Salaam ambapo dakribani vituo vyote walikuwa hawajapiga kura kutoka na kuratasi za kupigia kura kwa ngazi ya Urais kumalizika.
 Mbali na Kibamba Kasoro nyengine zimejitokea pia sehemu ya Bariadi ambapo napo maeneo mengi ya huko karatasi za kupigia kura kwa ngazi ya Udiwani zilikuwa zinakasoro.

 ENDELEA KUFUATILI FULLHABARI.BLOGS UTAPATA HABARI KAMILI.

Hakuna maoni