Zinazobamba

DK SLAA AENDA ZAKE MAREKANI,DHAMBI YA USALITI YAZIDI MTESA,SOMA HAPO KUJUA

ALIYEWAI pata kuwa Katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na MaendeleoChadema,DK wilbroad Slaa ameondoka tena na kwenda nchini Marekani,Mtandao huu umebaini,Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Dokta Slaa ambaye alitangaza kuachana na siasa pamoja na  kujivua nafasi zote za uongozi alizokuwa nazo Chadema kwa kile anachokisema kutolizishwa na chama hicho wakati wa kumteua mgombea anayekubalika nchini kwa sasa Edward Lowassa kwenye nafasi ya Urais,
         Taarifa kutoka vyanzo vyetu vya habari zinasema Katibu huyo ameondoka nchini marekani kuendelea na mapumziko yake,huku akipisha uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika siku 7 kutoka sasa,
        Chanzo chetu hicho kinasema kwa sasa Dk Slaa ametimkia marekani huku akiwa na lengo moja ni la kuombea mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM,John Magufuli achaguliwe nafasi hiyo ili aweze kumteua Dk Slaa kwenye nafasi yeyote kubwa nchini.
       “Huyu bwana (DK Slaa) nafsi inamsuta kubaki nchini,jinsi alivyotegemea kuondoka yeye chadema ingepotea kumbe kaja kupotea yeye kwenye ramani ya siasa,”
    “Huku akijijua nafasi yake ndani ya chadema ilivypambana kukijenga chama hicho,ila ndio hivyo amekubali kupanda bei,ndio hivyo sahivi anangojea hisani kwa huyo anayempigiea debe Magufuli awe Rais  ili amteua hata ukuu wa mkuo”
          Kuondoka huku kwa Dokta slaa kunakuwa ni kama mara ya pili baada ya mara ya kwanza pale alipotangaza kujivua nafasi hizo kubwa ndani ya chadema aliondoka marekani,

       Ambapo Duru mbali mbali zinasema sababu ya Dk Slaa kuondoka ilitokana  na kile kinachotajwa kuwa inatokana kukimbia mashambulizi yaliyotolewa na wale aliwatuhumu kwa uongo mara pale alipojiuzulu.

No comments