CHADEMA YAUPONDA MDAHALO WA TWAWEZA,YASEMA LOWASSA HAWEZI SHIRIKI MIDAHALO YA "KIKANJANJA"SOMA HAPO KUJUA
CHAMA cha Demokrasi na
Maelendeleo (Chadema), kimetoa ufafanuzi wa suala la kutohudhuria kwa mgombea
urais kupitia mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kwa tiketi ya
chama hicho, Edward Lowassa katika Mdahalo wa Mgombea urais uliondaliwa na
Taasisi ya Twaweza pamoja na Tanzania Media Foundition. Anaandika
Faki Sosi … (endelea).
Hayo yameelezwa na Afisa Habari wa Chadema,
Tumaini Makene alipokua akijibu maswali ya waandishi wa habari katika ufunguzi
wa kituo kipya cha mikutano ya waandishi wa habari cha UKAWA,amesema kuwa
mdahalo huo haukidhi viwango vya ubora wa kuweza kuwapima vizuri wagombea
Akitaja vigezo vya
midahalo mikubwa ya mgombea urais amesema kuwa kigezo hawakuweka kigezo cha
wagombea kuulizana maswali,pia waandaaji hao hawana sifa ya kuandaa midahalo
kutokana kukosewa imani na umoja huo kwa kutoa tathimin zinazobeba upande mmoja
ambao ni wa Chama Cha Mapinduzi, (CCM).
Aidha Makene
aliwashangaa waandaji wa midahalo ambao tayari wameshajipambanua kuwaunga mkono
wagombea wengine halafu wanajificha katika pazia kuandaa midahalo ili kuhadaa
umma wa watanzania.
Hivi karibuni, Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kilimkataza mgombea wake Edward Lowassa
kuhuduria mkutano ulioandaliwa na Taasisi Watendaji wakuu wa makampuni (CEORT)
baada ya Mwenyekiti wake Ali Mfuruki kujipambanua kumuunga mkono John Magufuli
mgombea wa urais kupitia Chama cha Mapinduzi.
Mmoja ya waandaaji wa
mdahalo wa marais, akiwa katika kampeni ya mmoja wa mgombea Urais
“Nchi ya marekani na
nchi nyengine wanakuwa na Taasisi maalum zenye kuamika ambazo huanda midahalo
iliyo bora na yenye vigezo bila kukibeba chama fulani” amesema Makene.
Wiki hii katika Ukumbi
wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere kulifanyika mdahalo uliorushwa na
kituo cha televisheni cha Star tv uliohudhuliwa na wagombea wanne ambao ni
Chief Lutaselo Yemba wa chama cha Allience For Democry Change (ADC), Anna
Mghwira wa ACT-Wazalendo, Maximilan Lyimo wa Tanzania Labour Party (TLP) na
Mgombea aliyechelewa kufika kutokana na alichodai ni kuchelewa njia, Hashim Rungwe
wa Chama Cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA).
Hakuna maoni
Chapisha Maoni