MBOWE AZUSHIWA,CCM YATUMIA MAGAZETI YAKE KUTUNGA UONGO,MAKENE ASEMA YAPUUZENI KAMA UKOMA,SOMA HAPO KUJUA
CHAMA cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimekashangwazwa na tuhuma za uongo na
uzushi zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari dhidi ya Mwenyekiti wa chama
hicho Freman Mbowe za kuhamisha fedha katika akaunti za nje. Anandika Faki Sosi … (endelea).
Akizungumza
na waandishi wa habari msemaji wa chama hicho, Tumaini Makene ameeleza kuwa
hakuna sheria inayomkataza mtu kutofanya biashara na kuhamisha fedha zake
binafsi.
Akitaja vyombo hivyo
amesema kuwa ni Magezeti ya Jambo Leo, Uhuru na Raia Tanzania ambayo
yanaonaonekana kuwa na maslahi ya kisiasa kwani habari hiyo imeonekana
kuhaririwa na mhariri mmoja kutokana na kutokuwa na uthibitisho wala ushahidi
wa upande wa pili.
“Mimi ni
mwandishi mwenzenu, naifahamu taaluma hii, ukisoma habari hiyo utaona inafanana
kwa kila mstari, nukta hadi koma, inaelekea iliandikwa na mwandishi mmoja na
kusambazwa kimaslahi kwa magazeti yote matatu na wahariri wakapachika” alisema
Makene.
Amesema kuwa
mwenyekiti huyo ni mfanyabiahara wa kimataifa ambaye anafanya biashara zake
halali nje na ndani ya nchi zinazojulikana na serikali, aidha magazeti hayo
yanaandika ili kuwaondoa wananchi kwenye ajenda kubwa ya Uchaguzi sababu chama
cha Mapinduzi kimeelemewa.
Leo Magazeti
matatu yaliandika kuwa Freeman Mbowe, anatuhumiwa kuhongwa ili kumpitisha
Edward Lowassa, kuwa mgombea urais wa chama hicho, yakimtuhumu kufanya uhamisho
wa mabilioni ya fedha kwenye akaunti yake hivi karibuni.
Kwa mujibu wa
Uhuru, Jambo Leo na Raia Tanzania yaliandika kuwa zilikuwa ni njama za Mbowe,
kufanya uamuzi wake wa kumpitisha Lowassa kuwania urais pasipo kushindanishwa
na mtu ndani ya chama chake na ndani ya muda mfupi, uamuzi unaodaiwa kukigawa
chama hicho,
Hata hivyo gazeti
la Mawio limenukuliwa mara kadhaa likiweka wazi kuwa hakuna mgawanyiko kwenye
Chadema isipokuwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho Dk Willbrod Slaa ndiye
aliyenunuliwa kupitia mke wake Josephine Mushumbusi, na baada ya hapo wamekuwa
wakifanya juhudi kubwa kukisaidia CCM ili kudhoofisha Chadema.
Magazeti hayo kwa
pamoja yaliandika kuwa Mbowe anahamisha hela hizo wakati wagombea kupitia chama
chake hawana hela, hata hivyo Makene alifafanua kuwa hakuna sera ya Chadema
kutumia pesa za mtu binafsi na biashara zake kwa ajili ya kusaidia wagombea,
isipokuwa hela zinazopatikana kutokana na ruzuku hutumika kwa shughuli za chama
na hesabu zake zinajulikana.
Habari hii
kwahisani ya Mwanahalisi oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni