Zinazobamba

BARAZA LA MITIHANI LATANGAZA MATOKEO YA DARASALA LA SABA LEO,MAMBO NI YALE YALE,SOMA HAPO KUJUA

pichani ni Katibu mkuu wa Baraza la mitiani nchi NectaDK,Chalse Msonde

BARAZA la Mitihani la Tanzania (NECTA), limetangaza matokeo ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi uliofanyika Septemba 9 hadi 10, mwaka huu ambapo mkoa wa Katavi umeibuka kidedea katika orodha ya mikoa kumi iliyoongoza Kitaifa, huku shule bora ikiwa ni WajaSpring (Geita).Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo,
Pia katika matokeo hayo jumla ya watahiniwa 775, 273 wa Shule za Msingi walisajiliwa kufanya mtihani huo, wasichana ni 413, 966 sawa na asilimia 53.40 na wavulana 361, 307 sawa na asilimia 46.60.Ambapo watahiniwa 683 walikuwa na uoni hafifu.
     Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mtenda (NECTA), Dk.Charles Msonde amesema watahiniwa 763, 606 sawa na asilimia  98.50 ya waliosajiliwa walifanya mtihani, ambapo wasichana 408, 990 sawa na asilimia 98.78 na wavulaana 354, 706 sawa na asilimia 98.17, huku watahiniwa 11, 667 sawa na asilimia 1.50 hawakufanya mtihani huo.
      Amesema jumla ya watahiniwa 518, 034 sawa na asilimia 67.84 kati ya 763, 606 waliofanya mtihani huo wamefaulu, ambapo wasichana ni 264, 130 sawa asilimia 64.60 na wavulana ni 253, 904 sawa na asilimia 71.58.
“Kwa mwaka jana watahiniwa waliofaulu ni asilimia 56.99 hivyo kuna ongezeko la ufaulu kwa asilimia 10.85,”amesema.
Dk.Msonde amefafanua kuwa mbali ya mkoa wa Katavi kuibuka kidedea, pia mikoa mingine iliyofanya vizuri ni Dar es Salaam asilimia 83.17, Mwanza (82.14), Kilimanjaro (80.13), Arusha (79.67) na Geita (78.52).Pia Kagera (76.80), Tanga (76.71), Njombe (75.65), na Iringa (73.25).
 Pia amewataja watahiniwa kumi waliofanya vizuri Kitaifa, ni Jaffar Matange na Karimu Seyn (Shule ya Hazina-Dar es Salaam), Teddy Range, Paulina Gercas, Nyegero Amos, Juster Mgarula, Janeth George (Shule ya Mugini Mwanza).
Pia Ibrahimu Kondo (Rocken Hill-Shinyanga), Godbless Hhayuma, David Steven Mtalemwa( te Twibhoki-Mara).
“Katika ufaulu huo kuna wasichana kumi bora kitaifa, ambapo saba kati yao wametoka shule ya Mugini Mwanza na watatu wametoka Twibhoki na Little Flower mkoani Mara, kwa upande wa wavulana wanne wanatoka Shule ya Hazina Dar es Salaam, wanne kutoka Rocken Hill-Shinyanga na watatu kutoka Twibhoki-Mara,”amesema
Amezitaja shule kumi bora alisema ni Waja Spring (Geita), Enyamai, Twibhoki, Little Flower(Mara),  Alliance, St.Caroli,  Mugini (Mwanza),Rocken Hill na Palikas (Shinyanga) na Karume (Geita).
Pia Dk.Msonde amezitaja shule kumi ambazo hazikufanya vizuri ni Mwashigini(Shinyanga), Mabambasi(Simiyu), Mwangu(Lindi), Mohedagew, Njoro (Arusha),Gomhungile (Dodoma), Makole (Tanga), Morogoro na Koloni (Morogoro).
Hata hivyo, ameeleza kuwa katika matokeo hayo ufaulu katika masomo yote umepanda kwa asilimia 4.61 na 17.22 ikilinganishwa na mwaka 2014.
Pia amesema watahiniwa wamefaulu zaidi katika somo las Kiswahili ambapo ufaulu ni asilimia 77.20 na somo waliofaulu kwa kiwango cha chini zaidi ni Kiingereza asilimia 48.56.
“Baraza linatoa wito kwa walimu na wanafunzi kuendeleza juhudi katika ufundishaji na ujifunzaji katika masomo yaliyofayika vizuriili ufaulu wake uweze kuimarika zaidi katika miaka ijayo,”amesema.
Aidha, amesema Maafisa elimu wa mkoa, wilaya na wadhibiti ubora wa elimu wanahaswa kufanya ufuatiliaji katika kuhakikisha kuwa ufundishaji unatiliwa mkazo ili kuongeza kiwango cha ufaulu.


No comments