RAIS KIKWETE LAWAMANI TENA,APEWA SAA 48 ZA MWISHO ZANZIBAR,SASA NI KUSUKA AU KUONYOA,SOMA HAPO KUJUA
![]() |
| Mgombea wa Urais Zanzibar kwa tiketi ya CUF, Maalim Seif Sharrif Hamad |
RAIS Jakaya Kikwete ameingia kwenye lawama nzito baada ya kutuhumiwa kutumia madaraka yake kutaka
kumpokonya ushindi Mgombea wa Urais kupitia chama cha wananchi CUF ambaye
anaungwa mkono na vyama vya UKAWA,Maalim Sef Sharif Hamaad.Mtandao huu
unaripoti.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Taarifa kutoka Dar es Salaam na Visiwani Zanzibar
zinasema kitendo cha mwenyekiti wa wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) bwana Jecha Salim Jesha kufuta uchaguzi wote na
kutangaza kufanyika tena ndani ya siku 90 kwa kile anachokisema uchaguzi
huo ulikuwa na kasoro lukuki,kumeingiza idara ya Rais kwenye kashfa.
Kwani Kitendo hicho cha Jesha kufuta
uchaguzi huo kinakwenda na kinyume na sheria za nchi kutokana na Mwenyekiti
huyo kutokuwa na mamlaka yeyote ya kisheria ya kufuta uchaguzi huo ambao inadaiwa
mgombea wa CUF alikuwa ameshinda nafasi ya Urais ya serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar baada ya kumwacha kwa mbali mpinzani wake Dk Mohamed Sheni.
Kwa mujibu wa mtoa taarifa wetu aliyoko ndani
ya ZEC ameumbia mtandao huu kuwa,kitendo alichokifanya Jecha cha kufuta
uchaguzi huo umetokana na yeye mwenyewe huku akidaiwa kushinikizwa na kigogo
mmoja wa juu wa chama cha Mapinduzi CCM.
“Ujue hapa tunapoelekea lazima damu itamwagike,maana leo viongozi wote
akiwemo Dk Sheni,Rais Kikwete wamekaa kimya wana mwacha Jesha anafuta uchaguzi
pasipo hata kumkemea, huko wote tukifahamu kuwa hakuna kipengele chechote cha
Katiba kinachompa mamlaka hayo Jesha,”
Amesema wao wanamtuhumu Rais Kikwete
kuhusika kwake inatokana na yeye kunyamazia au naye kuhusika kwa moja kwa moja
kutokana na kitendo cha kumfumbia macho Mwenyekiti huyo wa ZEC kuvunja katiba
ya nchi kwa kufuta uchaguzi huo,
Amesema Idara ya Urais ni ingetakiwa
kusimamia na kuilinda katiba ya Jamhuri ya Muungano lakini cha ajabu hakuna
hata kalipio kutoka wa Rais Kikwete kwa mwenyekiti huyo Jambo linalotia shaka
uwenda nayo idara ya Rais inahusika.
Kuibuka kwa tuhuma hizi kwenye Idara ya Ikulu, kunakuja ikiwa ni siku
moja baada ya Mwenyekiti wa kamati ya Uongozi ya CUF,Twaha Issa Taslima kuibuka na kusema
kwamwe chama chake akitashirikia kwenye uchaguzi mwengine kutokana na
mwenyekiti wa ZEC kutokuwa na mamlaka kamili ya kufuta uchaguzi.
Akizungumza na
waandishi wa habari jana,Taslima amesema jambo linaloshangaza ni kuona mwenyekiti wa ZEC kutangaza
kufuta uchaguzi bila ya kuwashirikisha makamishna wake,
“Hili linathibitishwa na taarifa ya vyombo vya habari iliyotolewa na makamishna
wa zec kukanusha kuhusika na uamuzi huo wa mwenyekiti wa zec,ambapo hatua hii
ni uvunjwaji wa katiba ya Zanzibar (1984) ibara ya 119(10) inayotaka
vikao vya ZEC kuhudhuriwa na mweyekiti na makamu mwenyekiti na wajumbe wane4 na
uaamuzi kuungwa mkono na walio wengi”amesema Taslima.
Kuibukua
huko kwa CUF kunakuja ikiwa ni teyari mataifa ya Ulaya,yakiwa yakikipinga kitendo
cha ZEC kufuta uchaguzi nao wao wakiishinikiza ZEC kumalizia kutangaza matokeo
hayo huku wakisema hakuna dosari yoyote iliyojitokeza kwenye uchaguzu huo kwani
uchaguzi wote ulifanyika kwa uhuru na haki.
Mbali na
ZEC kufuta uchaguzi wa Zanzibar kunazidi ibua mashaka baada ya Mwenyekiti wa
Tume ya Taifa ya Uchaguzi.NEC,Jaji Mstaafu Damian Lubuva kulipinga jambo hilo na kusema ZEC haina
mamlaka ya kufuta uchaguzi huo,
Sanjari na
Lubuva,naye Mwanasheria mkuu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema,Tundu
Lissu ameishukuia ZEC kwa kusema haina mamlaka hayo kisheria huku akiwataka
Wazanzibar kudai haki yao barabarani.
Mjadala
huu,unafunga na Maalim Sef mwenyewe baada ya kutoa saa 24,ZEC iwe imemtangaza
mshindi badara yake atawaachia Wazanzibar wenyewe waamue,
Amesema amefanya jitihada za kutosha kutaka
kulimaliza suala hili,ila imeshindikana baada ya kumpigia simu Rais Kikwete
pamoja Rais Sheni huko wote kwa pamoja simu zao kutopokelewa.
Amesema machafuko yakitokea asije akaja kulaumiwa
mtu

No comments
Post a Comment