DK SLAA ATELEKEZWA,SASA ATUPWA RASMI, WATU WA USALAMA WASEMA HAWANA KAZI NAYE TENA,SOMA HAPO KUJUA
![]() |
pichani ni aliyewai pata kuwa Katibu mkuu wa Chadema,DK Slaa |
IKIWA ni siku
mbili tangu kutangazwa kwa mshindi wa mbio za Urais 2015, na siku moja tangu
John Magufuli kukabidhiwa cheti maalumu cha ushindi watu wanaodaiwa kuwa ni
usalama wa Taifa wameanza kuwaandama watu. Anaandika Josephat Isango … (endelea).
Wakizungumza
kwa kujiamini, watu hao wanaojidai kuwa maofisa wa usalama walikutwa kwenye
hoteli moja iliyopo maeneo ya sinza jijini Dar es salaam.
Maofisa hao
walijiapiza kuwa watu waliokuwa vinara wa kuwatukana Usalama wa taifa kwa
kipindi kirefu na kusababisha usumbufu sasa watakiona.
Mmoja aliyekuwa
akitajwa na wenzake kwa jina la Yusufu alinukuliwa akisema “Gwajima ametutukana
sana, sasa tutashughulika naye, lakini Dk Willbrod Slaa ambaye awali alikuwa
akitutukana sasa japo yupo upande wetu tutamtelekeza maana hatusaidii tena.
Kuripotiwa habari
hizo kunakuja takribani mwezi mmoja na wiki tatu tangu Gwajima alipowaonya
maofisa hao kuwa wamekuwa wakitumika vibaya.
Gwajima alisema hayo
katika hoteli ya LandMark Septemba 8 mwaka huu alipokuwa akimjibu aliyekuwa
katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) aliyejitokeza kwa
waandishi kudai kuwa kupokelewa kwa Edward Lowassa kwenye Chadema kulimfanya
yeye ajiondoe Chadema, madai ambayo Gwajima alisema sio ya kweli na kuweka wazi
kuwa Dk Slaa alikuwa anatumiwa
vibaya na usalama wa Taifa.
Katika hatua nyingine vijana hao wa Usalama walijiapiza kuwa
sasa katibu mkuu huyo hana madhara kwa siasa na ameshindwa kukisaidia Chama cha
Mapinduzi (CCM) kuisambaratisha Chadema katika uchaguzi ambao CCM walikuwa
wameelemewa.
Habari hii kwahisani ya mwanahalisi oline
No comments
Post a Comment