Zinazobamba

HABARI KUBWA LEO-LOWASSA AIPA MAJANGA ITV,TCRA YAILIMA,SOMA HAPO KUJUA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj1usN5ShyiMFa6U6jG54I8hbY4GLJ-PlelC6_I6aYW_hgCVxY68bAKJ2AcLPrfxVI1gz7LLhwLiZTIWbJD8-BtsucFquoGxrCLXMl1Ds0Mx8Zds9y61Iql8Q8eq_Az5rQEQNfyzApROrU/s1600/SAM_0783.JPG

EDWARD Lowassa ni kama ameanza kuipa majanga kituo cha Televisheni Cha ITV ndivyo naweza kusema baada ya Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) kukitaka kituo hicho kuomba radhi mara mbili mfululizo kwenye taariifa zake za habari pamoja na kupewa onyo kali baada ya kukiuka sheria ya utangazaji nchini ya Mwaka 2005.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
           Hukumu hiyo ilitolewa leo jijini Dar es Salaam na kamati ya maudhui ya utangazaji, katika ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Margaret Munyagi (pichani) wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari ambapo  Muyangi  amsema kamati hiyo imebaini kituo cha  ITV kulikiuka sheria hiyo ya utangazaji nchini kwa kurusha taarifa ambayo ingeweza kuleta machafuko nchini.
             Amedai katika kipindi cha Habari zilizotufikia mda huu kilichorushwa siku ya Jumatatu ya tarehe 10 mwezi huu majira ya saa 2.22 asubuhi ambapo katika kipindi hicho kilirusha taarifa kuhusu  “Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limepiga marufuku maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema wakati wa kumsindikiza Lowassa kwenda kuchukua fomu ya Urais.
         Amesema katika kipindi hicho Mtangazaji wake alisikika akisema Jeshi hilo limezuia maandamano hayo baada ya kubaini yanauvunjifu wa amani huku Mtangazaji huyo akimnukuu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova akidai ndipo amesema hivyo,Wakati taarifa hiyo ilikuwa ya upotoshaji kwani jeshi hilo alikuwa alijasema taarifa hizo..
           Be Muyangi  amesema baada ya ITV kurusha taarifa hiyo ya kwanza juu kuzuiliwa  huko kwa maandamano, ndipo siku hiyo hiyo  tena katika kipindi hicho cha Habari zilizotufikia mda huu majira ya saa tatu asubuhi kilirushwa taarifa inayosema Jeshi la Polisi limeruhushu maandamo ya Chadema kutoka Makao makuu wa Chama chaWananchi CUF Buguruni Jijini Dar es Salaam kwenda Ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC amedai katika taarifa hiyo ilisikika sauti ya Kamanda Kova juu ya kuruhusu maandamono hayo,tofauti na taarifa ya kwanza haikuweka uthibitisho wa Kamanda Kova.
           Amesema Baada ya Mamlaka hiyo kubaini makosa hayo,Kamati hiyo iliwasiliana na Mkurugenzi wa Itv Be Mhavile na mkurugenzi wa Redio one Deogratus Rweyunga pamoja na Mhariri wa ITV Steven Chuwa.
         Ili kutaka  ufafanuzi ambapo wote kwa pamoja walikili kosa hilo huku wakisema Mtangazaji huyu alitoa taarifa kwenye Mitandao ya Kijamii ambayo ilikuwa inakataza maandamano hayo ambapo alishindwa  kuithibitisha kama taarifa hiyo kama ni ya kweli au la.
            Aidha, Be Muyangi amesema baada ya Kamati hiyo kusikiliza pande zote,ndipo wakatoa hukumu kwa kupitia sheria ya Utangazaji ya mwaka 2005 ambayo inakataza kituo chohote cha Utangazaji kurusha taarifa zinatazoleta mchanganyiko katika jamii,

       Ndipo wakatoa  hukumu ya kuitaka ITV kuomba radhi mara mbili kwenye taarifa za habari ya asubuhi na jioni kwaanzia hukumu hiyo ilipotolewa leo na kupewa onyo kali.