WAZIRI MWAKYEMBE ANAWEWESEKA NA LOWASSA,SOMA HAPO KUJUA
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Harrison Mwakyembe |
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk.
Harrison Mwakyembe, amewataka wanasiasa kuacha kujificha mgongoni kwake kwa
lengo la kumshambulia Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Richmond, Edward
Lowassa. Anaandika
Mwandishi Wetu … (endelea).
Dk. Mwakyembe ametoa onyo hilo leo wakati
akihojiwa na kituo cha redio cha Clouds FM kuhusu taarifa iliyosambazwe kwenye
mitandao ya kijamii ikionesha imetoka kwake kwamba atapambana na Lowassa katika
sakata la Richmond.
“Taarifa ile
haikuwa ya kwangu, ni upuuzi. Mnanijua kwamba huwa sikurupuki. Mimi ni
waziri wa Serikali ambaye naheshimu wadhifa wangu, hivyo siwezi kuandika mambo
kama hayo. Nilipigiwa simu hata na wenzangu wakiniuliza mbona nimeandika maneno
makali,”amesema.
Kwa mujibu wa Dk.
Mwakyembe, hana sababu ya kuendelea kujadili swala la kashfa ya Richmond kuhusu
Lowassa.
“Kama ni suala la
kashfa ya Richmond, jamani mbona tulimtanguliza Mungu? Tulifanya kazi yetu kwa
haki na ripoti ya Bunge ipo. Sasa hakuna haja ya unafiki…unafiki wa watu kutaka
kumsema Lowassa halafu wanajificha mgongoni kwangu,” amesema.
Amesema amekwisha
kamilisha hatua za awali za kutoa taaria katika mamlaka zinazohusika ikiwemo
Polisi Makao Makuu Kitengo cha uharifu wa kimtandao (Cyber Crime), Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA) ili waweze kubaini mtandao huo ambao ulianza
harakati zake tangu Lowassa atangaze nia.
“Sio uungwana
kuchezea majina ya watu wanaokosa ujasiri wa kuelezea hisia zao hadi watumie
majina ya watu wengine, mtandao huo nauona kuwa ni hatari,” amesema na kuongeza
kuwa huenda kwa sababu ya joto la uchaguzi ndio maana suala hilo likapewa msukumo.
Dk. Mwakyembe
ametamba kuwa, “nimedhamiria kukomesha tabia hii, nimekwenda Polisi Kitengo cha
Cyber Crime (Mkosa ya Jinai ya Mtandao) na TCRA, kulalamikia mchezo huu hatari
wa kihuni na tayari vyombo hivi vimeanzisha uchunguzi huu mkali, ili kubaini wahusika
wote wanaoandaa hizo taarifa na kuzituma kwenye sehemu mbalimbli na wanaozituma
sehemu nyingine hizo taarifa, lakini lazima tupeleke ujumbe ulio wazi kwa
sababu nchi yetu inaendeshwa kwa misingi ya sheria”.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni