PROF.MWANDOSYA,WASSIRA WACHUKUA FOMU ZA URAIS KWA MADAHA MAKUBWA,WAENDELEZA WIMBO WA KUMSAIDIA MTANZANIA,SOMA HAPO KUJUA
Mawaziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Profesa Mark Mwandosya (kulia) na Waziri wa Kilimo na Ushirika, Steven Wasira (kushoto) wakiteta na Kiongozi wa Upinzani Bugeni, Freeman Mbowe |
MAWAZIRI wawili katika Serikali ya Rais Jakaya
Kikwete- Stephen Wassira (Kilimo, Chakula na Ushirika) na Prof. Mark Mwandosya
(Ofisi ya Rais-Kazi Maalum), wamekuwa makada wa mwanzo kuchukua fomu za kuomba
uteuzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa
Oktoba mwaka huu. Anaandika
Dany Tibason … (endelea) .
Kama ambavyo wamejinadi wakati
wakitangaza nia, makada hao kwa nyakati tofauti baada ya kukabidhiwa fomu hizo
katika ofisi za Makao Makuu ya CCM- Dodoma, walizungumza na waandishi wa habari
ambapo Prof. Mark Mwandosya ameahidi kukomesha vitendo vya rushwa huku Wassira
akiahidi kufufua uchumi wa viwanda na kilimo ili kuondokana na jembe la mkono.
Akizungumza baada
ya kukabidhiwa fomu hiyo, Prof. Mwandosya ambaye aliambatana na mkewe Lucy,
amesema mbali na kukomesha vitendo vya rushwa na ufisadi, pia amejinadi kuwa
atahakikisha anaufanya uchumi wa Tanzania kuwa sawa na Bara la Ulaya.
Amesema kuwa,
amelazimika kuomba ridhaa ya Watanzania kwa ajili ya kuliongoza Taifa ambalo
kwa sasa linakabiliwa na changamoto lukuki ikiwa ni kutokana na umasikini ambao
umekithiri.
Prof. Mwandosya
amesema katika vipaumbele vyake ni lazima kuwa na uchumi ambao utamwezesha kila
mtanzania kuona anafaidi rasilimali za nchi.
“Tumeuona uchumi wa Ulaya, Asia na Marekani ulivyo mkubwa na
sasa Afrika kuna uwezekano mkubwa katika kipindi cha miaka 2025 au 2050 tukawa
na uchumi kama wa nchi hizo na tukaongoza kwa uchumi katika Bara la Afrika.
“Katika kuinua
uchumi natamani ifikapo kwaka 2025 au 2050 tukawa na uchumi imara katika dunia
ya sasa kutokana na kuwa na rasilimali nyingi ambazo nchi inazo kama vile
mafuta, gesi, mbuga na hifadhi pamoja na vyanzo vingine vya mapato ya
ndani,”amesema.
Ameongeza kuwa
“tukiimarisha uchumi ni wazi kuwa tutaondokana na suala la kuomba misaada
kutoka katika mataifa mengine jambo ambalo linaweza kusababisha kuwepo kwa
misaada yenye masharti magumu”.
Mbali na hilo,
amedai kuchukizwa na sera za watangaza nia kuchafuana na kusemana huku
wakiendelea kukisema vibaya chama chao pamoja na serikali.
Wassira
Baada ya kukabidhiwa
fomu yake, Wassira amewaeleza waandishi wa habari kuwa, anaamini ikiwa
ataingia Ikulu na vipaumbele vyake, atahakikisha anafufua uchumi wa viwanda na
kilimo ili kuondokana na jembe la mkono na badala yake kulima kilimo cha kisasa.
Amesema kuwa,
katika hatua nyingine ya kukuza uchumi, atawekeza zaidi katika kilimo cha
umwagiliaji badala ya kutegemea kilimo cha mvua ambacho wakati mwingine
kinaweza kusababisha kutokuwepo kwa chakula cha kutosha.
Kwa mujibu wa
Wassira, iwapo kilimo cha umwagiliaji kitapewa kipaumbele, ni wazi kuwa
kitapatikana chakula cha kutosha na kingine kwa ajili ya kuuza kwa nchi
nyingine za nje na kupata fedha ya kigeni.
Amesema “nikiingia madarakani ni lazima nijue viashiria vya
umasikini, kutatua matatizo ya ajira hususani kwa vijana kwa kuwawezesha
kujiunga katika vikundi mbalimbali ili kuwawezesha kupata mitaji na kuweza
kuzalisha ajira wao badala ya kusubiri kuajiriwa”.
Wassira ameeleza
kushangazwa na jamii ambayo imekuwa na tabia ya kuwashangilia na kuwashabikia
watu ambao wamekuwa wakifanya ufisadi na kuonekana kuwa watu hao ni hodari
zaidi.
Chanzo ni Mwanahalisi.oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni