Zinazobamba

HOT NEWS,SAMWEL SITTA NAYE VITANI URAIS CCM,ATOA DIRA BORA SANA,SOMA HAPO KUJUA


Na Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii, Tabora.
Waziri wa Uchukuzi,Samwel Sitta amesema kuwa anataka Urais wa miaka mitano kuweza kuivusha nchi katika kutokana na mambo yanayoonekana ikiwamo muungano,udini ,ungezeko la vijana.
      Sitta ameyasema hayo leo wakati akitangaza nia ya kugombea urais katika mkutano uliofanyika katika viwanja  vya Ikulu ya Chifu Fundikira Kata ya Itetemia  mkoani Tabora.

       Amesema mtu  yeyote makini ana nafasi ya Urais, hana budi   kuyapima mazingira ya taifa katika miaka mitano ijayo na kuzielewa changamoto zitakazokuwepo katika kipindi cha uongozi anachokusudia kuongoza.
       “Maoni yangu kipindi cha miaka mitano ijayo kina mwelekeo wa mifarakano katika  masuala ya muungano wetu; kutetereka  kwa mshikamano wetu kunatokana na chokochoko  za siasa za ushindani, udini  na  kupanuka kwa  tofauti ya kipato, ongezeko la kundi kubwa  hususani la vijana mijini  lisilo  na uhakika wa ajira na haya yote yanaashiria ongezeko la uhalifu”amesema Sitta.

        Amesema anamini kutokana na  mchanganyiko wa uzoefu  wa uongozi, unamuwezesha kukusanya  nguvu chanya za Watanzania ili kuyatanzua matatizo yanayotokana na changamoto zilizopo kwa kipindi cha sasa.

        Sitta amesema kugombea nafasi ya Urais wa nchi yetu si jambo jepesi.Linahitaji tafakuri ya kina ukizingatia kuwa nafasi hiyo ya uongozi inabeba matumaini ya watanzania wote milioni 47.
         Amesema Ili kukuza uchumi wa nchi kwa kasi  inayopunguza umaskini kwa haraka na  huku  tukijenga uwezo mkubwa zaidi wa bajeti ya serikali kutosheleza ubora wa  huduma za jamii kama vile afya, elimu na maji, hatuna budi kufanya jitihada za makusudi za kuubadili mfumo wa uendeshaji nchi uwe ni wa motisha kwa wazalishamali. 

         Mifumo ya nchi zilizopiga hatua kubwa za maendeleo duniani ni ile iliyoweka mazingira chanya ya kuaminiana baina ya serikali na sekta binafsi. Hali hii  haijatimia  hapa kwetu.
          Aidha Wafanyabiashara wakubwa wa ndani hawawekezi vya kutosha ndani ya nchi kuleta maendeleo ya haraka ya huduma, viwanda,kilimo na biashara. Baadhi yao, kwa hakika baada ya kuchuma fedha wanazihamishia nje ya nchi. Matokeo yake ni kwamba uchumi haukui kufikia kiwango cha kutosheleza vipato vya wakulima na wafanyakazi na wafanya biashara.Hatuna budi kujenga muafaka na  wafanyabiashara hususani wazawa wa nchi yetu. Kazi hii ina hatua mbili:

         Amesema wafanyabiashara watachukuliwa hatua kwa wasio waaminifu kwa kukwepa kodi, wanaotorosha fedha za kigeni na wanaoshiriki katika rushwa kubwa na biashara za magendo,kuwepo kwa mshikamano baina ya wafanyabiashara waovu na watendaji serikali kunachochea rushwa na kudumaza uchumi. Hali hii lazima irekebishwe.


Hakuna maoni