Wafanyakazi nchini wananyonywa kwa kutojua sheria-Utafiti wa kituo cha sheria.
Utafiti uliofanywa na kituo cha nsheria na haki za binadamu LHRC umebaini unyonyaji mkubwa katika sekta ya wafanyakazi sekta binafsi kufutia wimbi kubwa la watu kutofahamu sheria mbalimbali ikiwamo mkataba wa kazi.
Utafiti huo uliofanyika mwaka 2014 umebaini asilimia 99 ya wafanyakazi nchini Tanzania wanafanya kazi chini ya mikataba ambayo
hawana ulewa nayo juu ya mgawanyo wa majukumu na kazi zao wawapo kazini
Wakizindua Repoti ya taarifa ya haki za binadamu na
biashara ya mwaka 2014, wataalamu kutoka kituo hcho cha sheria na haki za binadamu wamebainisha changamoto mbalimbali zinazoendelea katika sekta ya biashara.
Uzaifu wa sheria umejikita katika maeneo ya Ardhi,jinsia, kodi na mamlaka huska ambazo kwa kiasi kikubwa tafiti zilijikita kuangalia hali halisi za haki za binadamu.
Takribani asilimia 99 ya wafanyakazi wa nchi hii mikataba yao imeonekana kukosa mchanganuo wa kazi majukumu yao, huku 25% walipewa mkataba hiyo bila makubaliano. Kutokana na nja na shida zao walikubali kupokea mikata hiyo ambayo n ya kinyonyaji
Aidha Wakili Flaviana Charles aliwaambia umma waliohudhulia kongomano hilo kuwa tatizo la mikataba ya kazi katika nchi bado n mikubwa. 28% ya wafanyakazi waliohojiwa walionyesha kutojua maana ya mkataba wa maneno na ule wa maandishi.
| Wadau mbalimbali wakikabidhiwa Nakala ya Taarifa hiyo mara baada ya kuzinduliwa leo |
Akifafanua mambo ambayo
yamegundukika katika tafiti ya report hiyo mmoja kati ya watafiti kutoka kituo
cha sheria na haki za binadamu FLAVIAN CHARLES amesema kuwa maswala ya mikataba
kwa wafanyakazi nchini yameendelea kuwa tatizo kubwa ambapo asilmia 99 ya
wafanyakazi wamekuwa wakifanya kazi katika mikataba ambayo haielezi wazi
majukumu yao halisi huku asilimia 25 ya wafanyakazi walisaini mikataba bila
kuwa na makubaliano maalum na waajiri wao.
Aidha swala lingine ambalo limeonekana kuibuliwa na utafiti huo ni hali ya ubaguzi wa walemavu katika maeneo ya ajira ambapo zaidi ya asilimia 70 ya walemavu wanabaguliwa katika maswala ya ajira jambo ambalo limeelezwa kuwa baya sana ikizingatia kuwa walemavu ni watu wanaohitaji msaada wa karibu ili waweze kusonga mbele.
Katika hatua nyingine Report
hiyo imeonyesha taifa kutafunwa na tatizo la ukwepaji wa kodi pamoja na
biashara ya magendo ambapo imeeleza kuwa nchini Tanzania asilimia kubwa ya
makampuni makubwa na wawekezaji wakubwa wenye uwezo wa kulipa kodi wamekuwa
wakipata misamaha wa kodi huku watanzania wa kipato cha chini wakishushiwa
mzigo huo kwa kuendelea kulipishwa kodi jambo ambalo limeelezwa kuwa linahitaji
marekebisho makubwa ili taifa liweze kunufaika na wewekezaji waliopo nchini.
| Picha ya pamoja na wadau mbalimbali walioshiriki katika uzinduzi wa Taarifa hiyo leo jijini Dar es salaam |
Akizungumza wakati wa
kuzindua Report hiyo GODLISTEN NYANGE ambaye ni Mkurugenzi wa Tafiti Tume ya sheria
haki za binadamu na utawala bora nchini ambaye alimuwakilisha mwenyekiti wa
tume hiyo amesema kuwa Report hiyo ya haki za binadamu katika bishara imegusa eneo
ambalo limesahaulika sana na mashirika mengi huku akisema kuwa itasaidia sana
kufichua maswala mbalimbali wanayokutana nayo wafanyakazi katika maeneo kazi
zao.
Katia hatua nyingine Wakili Flaviana amebainisha unyanyasaji ambao upo katika seta hiyo ya kazi, ambapo alisema unyanyasaji unaoongoza ni ulemavu, takribani asilimia 71.6 wanabaguiwa kwa misingi ya ulemavu wao
No comments
Post a Comment