Zinazobamba

TNGP YAVIKOMALIA VYAMA VYA SIASA,NI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU,SOMA HAPO KUJUA

pichani ni  Mwezeshaji wa warsha ya kuwajengea
 waandishi wa habari uelewa wa namna ya kuripoti habari za uchaguzi wa mwaka huu na habari za bajeti katika mrengo wa kijinsia Deogratius Temba
akitoa semina hiyo kwa wanahabari

Waandishi wa Habari kutoka vyomba mbali mbali vya Habari wakiwa
 kwenye Semina hiyo wakimsikiliza bwana Temb
a
MTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP), umesema katika kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kama hakutokuwepo na sheria na taratibu za uchaguzi wanawake na vijana watashindwa kupata uongozi.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo

     Hayo yamesemwa leo Dar es Salaam  na Mwezeshaji wa warsha ya kuwajengea waandishi wa habari uelewa wa namna ya kuripoti habari za uchaguzi wa mwaka huu na habari za bajeti katika mrengo wa kijinsia Deogratius Temba.

   Temba  amesema kuna dalili ndani ya vyama  zinaonesha kuwa wagombea  wanatumia kiasi kikubwa cha fedha kutangaza nia  hivyo kupelekea wenye kiasi kidogo kushindwa kutangaza nia hadharani kutokana na ufisadi huo.

     Ameongeza kuwa katika chaguzi nyingi zilizopita wanawake katika kinyanganyiro cha kugombea wameonekana kunyanyaswa na wagombea wakiume.

"Wanawake wameonekana kutolewa lugha za matusi ya kimwili na kupelekea jamii kutowaelewa hivyo lazima serikali isimamie vyema sheria na taratibu za uchaguzi kwa lengo la kukuza demokrasia wakati wa uchaguzi,"amesema


pamoja na hayo amebainisha kuwa wanawake wanapopewa nafasi za upendeleo ama viti maalum iwe kama chanzo cha kujikomboa katoka sehemu nyingine hususani kwenda kutetea jimbo kwa wabunge wengi.

     Hata hivyo amewataka wanawake wanaogombea nafasi mbalimbali kutojikita katika kufikiria ngazi za viti maalumu tuu bali wategemee kwenda kushindana na wanaume ndani ya ngazi za jimbo ili kuwawezesha wanawake wengine kugombea nafasI hizo



Hakuna maoni