HABARI KUBWA LEO, KINGUNGE ALIPULIWA,WASOMI WAMCHAKAZA,WASEMA LOWASSA ANAMMALIZA,SOMA HAPO KUJUA
Mwanasiasa mkongwe, Kingunge Ngombale Mwilu akimnadi Edward Lowassa |
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), sio taasisi tena,
kimegawanyika, kimeparanganyika na hakiwezi kuongoza tena. Anaandika Pendo Omary … (endelea).
Hali hiyo, imetajwa kudhihirishwa na
kitendo cha mwanasiasa mkogwe, mwenye ushawishi mkubwa ndani na nje ya CCM,
Kingunge Ngombale Mwiru kutamka hadharani kuwa “mbunge wa Monduli, Edward
Lowassa ndiye pekee anafaa kuwa Rais.”
Mbali na Kingunge
ambaye pia ni mwasisi wa TANU, pia wamo baadhi ya viongozi wa chama hicho ambao
ni wenyeviti wa mikoa na wilaya walijitokeza hadharani kuwaunga mkono watangaza
nia akiwemo Hamisi Mgeja, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga na Mgana Msindani
ambayeni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida.
Kauli hiyo imetolewa na wachambuzi mbalimbali wa siasa, wakati wa
mahojiano na Chanzo changu.
Akizungumza na
Chanzo hicho, Dk. Azaveli Lwaitama ambaye ni Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu
Shirikishi cha Josiah Kibira cha Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira amesema “ni
viashiria kuwa, CCM kimeondoka kwenye taasisi, kimetekwa nyara.”
“Taasisi inafanya
mambo yake kwa vikao. Kila mmoja anapaswa kupeleka maoni yake kwenye chama.
Kisha vikao vinafanya maamuzi.
“Kitendo cha Ngombare
Mwiru kusema Lowassa ndiye mtu pekee anayefaa kuwa rais, huu ni ushahidi
mwingine kwamba anakishinikiza chama kumteua Lowassa,” amesema Lwaitama.
Lwaitama amesema
wagombea wanaojinadi kwa vipaumbele vyao, wakati chama kina ilani yake, tayari
mgombea huyo ameshapanga hata watu wake atakao waweka serikali kutawala.
“Hii maana yake ni
utawala wa mtu fulani kutaka kutumia chama cha CCM, kuingia madarakani afanye
mambo yake,” ameeleza Lwaitama.
Aidha, Dk. Ditrik
Kajanangoma, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Shule ya Uandishi wa
Habari (IJMC) amesema, hatua hiyo inaonesha CCM hakina utaratibu wa kuendesha
mchakato wa kumpata mgombea.
“Kinguge hana tofauti
kubwa na marais wastaafu kwa hadhi yake na nafasi yake ndani ya chama na taifa.
Ushawishi wake ni mkubwa. Madhara yake kwa wagombea na wanachama wa CCM na
taifa, itaonekana amenunuliwa na kuingilia mchakato,” amesema Kajanangoma.
Mbali na kuonekana
kama viongozi hao wamenunuliwa, Kajanangoma amesema pia ni kuonesha kuchoshwa
na hali ya CCM, hivyo wameona wajitokeze mapema kuweza kumshawishi mtu
wanaedhani anafaa.
“Ni mara ya kwanza
kushuhudia haya tunayoyaona. Ni muhimu CCM kutumia udhaifu huu, badae waweke
muongozo na taratibu ili hali hii isijirudie,” ameeleza Kajanangoma.
Kwa upande wake,
Mwalimu wa sayansi ya siasa wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, Bashiru Ally
amesema ni muhimu kufanya udadisi na uchambuzi wa haya yanayojitokeza ndani ya
CCM.
“Ni muhimu kuangalia misukomo na misuguano
inayopelekea haya tunayoyaona,” amesema Bashiru.
Chanzo ni Mwanahalisi oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni