MAALIM SEIF NI MWISHO WA MATATIZO,AITEKA ZANZIBAR,POLISI WAIGWAYA NGUVU YA UKAWA,SOMA HAPO
SHUGHULI mbalimbali zilisimama kwa muda wakati
wa mkutono wa Chama cha Wananchi (CUF) uliohutubiwa na Katibu Mkuu wake, Maalim
Seif Sharif Hamad. Anaandika Mwandishi Wetu Zanzibar … (endelea).
Maalimu Seif ambaye tayari amechukua fomu
kugombea urais kupitia chama hicho, alihutubia maelfu ya wananchi na wakazi wa
Zainzibar kwenye Uwanja wa Kibandamaiti, visiwani humo.
Hali ilivyokuwa,
wakazi wengi wanaoishi karibu na uwanja huo walisimamisha shughuli zao na
kuungana na wananchi kutoka maeneo mbalimbali visiwani humo ili kuhudhuria
mkutanmo huo.
Katika mkutano
huo, Maalim Seif aliwaahidi Wazanzibar kubadilisha kisiwa hicho na kuwa kisiwa
chenye matumaini na fursa mbalimbali za kiuchumi tofauti na ilivyo sasa chini
ya utawala wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
“Nakusudia kuifanya
Zanzibar kuwa visiwa vya fursa za biashara na ajira kwa wananchi.”
Maalim Seif ambaye
tayari chama chake kimemteua rasmi kuwa mgombea wa nafasi ya urais visiwani
humo katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015.
Amesema, Zanzibar
inazo fursa nyingi za kuweza kunyanyua kipato cha wananchi, na kwamba ataweka
kipaumbele katika kuziibua na kuziendeleza fursa hizo.
Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
amesema katika kujenga mazingira bora ya uwekezaji, ataisimamia ipasavyo
Mamlaka ya vitega uchumi, ili kuondosha vizingiti vinavyokwamisha uwekezaji
nchini.
Amefahamisha kuwa
wapo wafanyabiashara wengi wa ndani na nje ya nchi wenye nia ya kuwekeza miradi
mikubwa ya kiuchumi, lakini wamekuwa wakipata usumbufu, jambo ambalo ameahidi
kulishughulikia muda mfupi baada ya kuingia madarakani.
Sambamba na hilo,
Maalim Seif amesema iwapo atachaguliwa kuiongoza Zanzibar, atahakikisha kuwa
Zanzibar inakuwa na shirika lake la ndege ndani ya kipindi cha mwaka mmoja, ili
kurahisisha shughuli za kibiashara ikiwemo Utalii.
Amesema hatua hiyo itakwenda sambamba na uboreshaji wa huduma za
viwanja vya ndege, ambavyo vitaweza kutoa huduma bora kitaifa na kimataifa.
Aidha amesema chini ya uongozi wake iwapo atapata ridhaa ya
kuongoza nchi baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015, ataitangaza Zanzibar kuwa
bandari huru, sambamba na kujenga bandari mpya itakayotoa huduma bora kwa
mwambao wa Afrika Mashariki.
Katika hatua nyengine Maalim Seif amesema anakusudia kuongeza
viwango vya mishahara kwa wafanyakazi wote, pamoja na kuzingatia maslahi ya
wastaafu na wazee wasiojiweza.
Akizungumzia kuhusu mafuta, Maalim Seif amesema anakusudia
kuanzisha Wizara ya Mafuta na Gesi ili kurahisisha uchimbaji wa nishati hiyo,
itakayoondosha hali ya umasikini katika visiwa vya Zanzibar.
Maalim Seif pia alizungumzia hali ya amani na utulivu nchini, na
kueleza kuwa amani ya kweli itapatikana iwapo vyombo vinavyohusika vitatoa haki
kwa wananchi wote.
Mapema akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa CUF Taifa,
Prof. Ibrahim Lipumba, amesema Baraza Kuu la Uongozi la CUF limeshawika
kumuidhinisha Maalim Seif kuwa mgombea Urais wa Zanzibar, kutokana na uwezo na
nia ya dhati ya kuwatumikia wazanzibari.
Amesema, viongozi waliopo madarakani wana dhamana na wajibu mkubwa
wa kuhakikisha kuwa uchaguzi mkuu ujao unafanyika katika hali ya amani,
sambamba na kuheshimu maamuzi ya wananchi katika uchaguzi huo.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni