ETI NCHEMBA ATAWAFUKUZA WALA RUSHWA SERIKALINI,SOMA HAPO KUJUA
Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba na mke wake Neema Mwigulu wakifurahia kukabidhiwa kwa fomu za kugombea urais. |
HEKAHEKA za makada wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) kuchukua fomu ili kuomba ridhaa ya kuteuliwa na chama hicho kugombea
urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, zimeshika kasi.Anaandika Dany Tibason … (endelea).
Leo Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Mwigulu Nchemba
amefungua pazia la uchukuaji fomu na kuahidi kufukuzwa wala rushwa wote katika
utawala wake.
Akiongozana
na mke wake, Mwigulu baada ya kukabidhiwa fomu, alikutana na waandishi wa
habari kwa lengo la kuulizwa maswali.
Kabla ya kuulizwa maswali Mwigulu amesema, akipata ridhaa ya kuwa
Rais wa Tanzania atahakikisha anakuza uchumi wa nchi kwa kufufua viwanda
na kuendeleza kilimo bora na kilicho na tija.
Pamoja na hivyo amesema, rasilimali za nchi atazitumia vizuri ile
ziwe neema kwa watanzania wote ikiwa ni sambamba na kukomesha matumizi mabaya
ya fedha.
“Katika uongozi wangu, nitakomesha kabisa matumizi mabaya ya fedha
na ikionekana viongozi au kiongozi amehusika katika hilo, atafukuzwa na
kufilisiwa mali zote.
“Kwanini kuwe na matumizi mabaya ya fedha wakati kuna mambo
muhimu hatujayakamilisha. Kuna shida ya madawati mashuleni, madawa hosptalini,
nitapambana na matumizi hayo ili kuboresha sehemu husika.” Amesema Mwigulu.
Katika awamu yake amesema, atapambana na tatizo la ajira kwa
vijana kwa kufufua na kuanzisha viwanda vingi hali itakayochochea ongezeko
la ajira nchini.
Amefafanua kuwa, katika awamu yake atapambana na rushwa na
ikibainika mtumishi wa umma anapokea au kutoa, atamfukuza madarakani.
Akijibu maswali ya waandishi lilihoji endapo akifanikiwa kuwa Rais
atalidhibiti vipi deni la Taifa .
Amesema, deni hilo limekuwa kwa kasi kubwa kipindi cha
uongozi wa Awamu ya Nne na hiyo yote ni kutokana na kukopa fedha kwa ajili ya
ujenzi wa miradi ya maendeleo zaidi ya 200.
Ametaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na ujenzi wa barbara,
bomba la gesi na ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
Aliyefuata kuchukua fomu mjini hapa ni Hakimu Mfawidhi wa Mahakama
ya Tanzania, Mussa Mwapongo.
Mwapongo amesema, hakuja kuongea isipokuwa ni kuchukuwa fomu tu na
kwamba atazungumza na waandishi kesho jijini Dare es Salamu.
Hata hivyo amesema, hana shaka na CCM kwani kina demokrasia na
utamaduni mzuri ambapo kinatoa nafasi kwa kila mwanachama anayedhani ana uwezo
katika kuwania nafasi hiyo kubwa.
Mwapango alishauri wagombea mwengine kwenda kuchukua fomu na
kuwataka kutokatishwa tamaa kwa namna yoyote na badala yake wasikilize sauti
zitokazo mioyoni mwao
CHANZO NI
MWANAHALISI OLINE
Hakuna maoni
Chapisha Maoni