TAARIFA MUHIMU KUHUSU ACT-WAZALENDO,TIZAMA HAPO UJUE WALICHOKUJA NACHO LEO,
Katibu Mwenezi wa ACT Wazalendo, Sabini Richard (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani). Kulia ni Said Sanani Naibu Katibu Mkuu Zanzibar |
JUNI 13 mwaka huu, Chama cha ACT-Wazalendo
kinatarajia kuzindua Azimio la Tabora mara baada ya kumaliza kikao chake cha
Halmashauri Kuu kitakachofanyika mkoani humo. Anaandika
Sarafina Lidwino … (endelea).
Akizungumzia kikao hicho kitakachofanyia
kwenye Ukumbi wa Community Center, Katibu Mawasiliano na Uenezi Taifa, Sabini
Richard amesema, lengo la kikao hicho ni kukamilisha hatua za kuliendea azimio
hilo.
Na kwamba, kikao
hicho kitapitisha kalenda ya Uchaguzi Mkuu pamoja na mikakati mbalimbali
inayohusu chama hicho katika kuelekea uchaguzi ujao baadaye mwaka huu.
“Kichama, wiki hii
tumeiita ni wiki ya Azimio la Tabora kwa kuwa, Mkutano Mkuu huu ni wa
kihistoria na utafanyika huko, ukiwa na ajenda kuu tatu muhimu
sana,” amesema Richard.
Amezitaja ajenda
hizo kuwa ni pamoja na kupokea na kujadili taarifa ya ziara katika mikoa 10
iliyofanyika Aprili mwaka huu, pili; kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji
wa oparesheni ya Majimaji.
Tatu ni kupokea,
kujadili na kupitisha Azimio la Tabora linalohuisha Azimio la Arusha
litakaloongoza utekelezaji wa siasa ya ujamaa wa kidemokrasia ya Chama cha ACT.
Amesema, “tumeamua
kufanyia mkutano huu mkuu Tabora tukienzi historia ya mkoa huo katika
ukombozi wa Taifa letu ambapo matukio makubwa ya ukombozi yalifanyika.”
Aidha amesema, baada
ya kumalizika kwa kikao hicho, Juni 14 chama kitaanza ziara katika mikoa sita,
ambayo ni Geita, Kagera, Kasulu, Kigoma mjini, Katavi, Rukwa na Mbeya.
Richard ametoa wito
kwa wakazi wote wa Tabora na mikoa mingine, kuhudhuria mikutano yote
itakayofanyika ili kukiunga mkono chama hicho.
Chanzo ni Mwanahalisi oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni