ETI MEMBE ASEMA ATAKUZA SEKTA YA AFYA,AMPIGA KIJEMBE LOWASSA,SOMA HAPO KUJUA
Mama Dorcas Membe mke wa Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe,
akimpongeza Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi, Ali Mtopa
WAZIRI wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (62) leo ameingia katika safari ya
watangaza nia ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) huku kipaumbele chake
ikiwa ni afya. Anaandika Pendo Omary … (endelea).
Membe ambaye ni Mbunge wa Jimbo Mtama (CCM),
ametangaza nia hiyo katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya CCM mkoani
Lindi.
Membe amesema
“nimejipima, nimetuma timu yangu kote nchini kufanya uchunguzi kama nakubalika
na vigezo vilivyowekwa na chama navitekeleza.
“Nimerizika kwamba,
nimetekeleza vigezo vyote, nina elimu ya kutosha,nina uzoefu ndani ya chama,
nina uzoefu mzuri serikalini na tasisi za kimataifa na nina uadilifu wa
kuzaliwa nao ambao siwezi kuuacha,” ameeleza Membe.
Akieleza kuhusu
vipaumbe ambavyo atashughulikia iwapo atapewa ridhaa na Watanzania ya kuiongoza
nchi baada ya kupitishwa na chama chake, Membe amesema “nataka nigeuze, nataka
madawa na huduma za hospitali ziwafuate wananchi pale walipo.”
Mbali na afya Membe
ametaja kipaumbe kingine kuwa ni kuboresha uchumi wa viwanda unaobebwa na
kilimo.
“Huu ni wakati mwafaka kwa sababu ya Mikoa ya
Lindi na Mtwara kumegundulika gesi. Lengo lake ni kubadilisha uchumi tulionao
kuupeleka kwenye viwanda. Viwanda vya kuajiri vijana, kuongeza tija kwa mazao
ya wakulima ili kuuza bidhaa zilizotengenezwa na kusindikwa nchini,” amesema
Membe.
Kuhusu utawala bora
Membe amesema, Tanzania inakabiliwa na mauaji ya albino, vitisho vya ugaidi na
dawa za kulevya huku akiahidi kupambana na wale wanaohatarisha amani ya nchi.
“Tutaimarisha vyombo vya usalama hasa jeshi la
polisi kwa kulipatia vifaa vya kisasa ikiwemo viona mbali,” amesisitiza Membe.
Ameeleza kuwa,
atahakikisha anaweka utaratibu ambao mtu anaetoa rushwa hatashitakiwa iwapo
atatoa taarifa kuhusu mtu aliyepokea rushwa. Pia amevitaka vyombo vya habari
kufichua na kuandika habari za rushwa ili serikali ichukue hatua.
Pia amesema, iwapo
atakuwa Rais atahakikisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar hauvunjwi kwa
namna yoyote.
“Muungano wetu ni wa
kipekee katika bara la Afrika na duniani. Wapo watu Zanzibar wanakebehi
mapinduzi. Hawathamini mapinduzi yaliyomwokoa mtu mweusi. Nitadumisha na
kuthamini mapinduzi ya Zanzibar. Lazima kutetea masuala ya Zanzibar kiuchumi na
kiutamaduni. Lazima tutambue upekee wa Zanzibar.
Amesema, serikali
itakayoudwa chini ya uongozi wake itahakikisha inaongeza mapato ya Zanzibar ili
iweze kwenda sambamba na uchumi utakaobebwa na viwanda na kilimo.
“Sitamvumulia mtu yoyote atakaeleta jaribio la
kuangusha muungano na kuuvunja muungano,” amesisitiza Membe.
Aidha amesema viwanda
vidogovidogo, kampuni kubwa, makampuni binafisi na mashirika yasiyo ya
kiserikali hayajapewa uzito ili kuweza kuajili. Serikali haitoi taarifa ya
kutosha na kushirikiana na sekta binafsi tuweze kusaidiana.
Kuhusu kuboresha elimu,
Membe amesema kufikia mwaka 2020 atahakikisha vyuo vya ufundi vinaanzishwa kila
wilaya ili vijana waweze kupata ujuzi ili badae waweze kujiali wenyewe.
Katika kuboresha
michezo na sanaa, Membe amesema atahakikisha vyuo vinajegwa, kutoa ruzuku kwa
vyuo binafsi na kuhakikisha wasanii na wanamichezo wanapata haki miliki.
Uzoefu ndani ya chama
Mwaka 1977 – alijiunga
na CCM akiwa na umri wa miaka 22.
Mwaka 2007 -2012 –
Katibu wa Siasa na Mambo ya kimataifa ndani ya CCM.
Mwaka 2007- 2012
– Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM.
Mwaka 2007 -2015
– Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM.
Uzoefu ndani ya
serikali
Mwaka 1978 – Afisa wa
Idara ya Usalama wa Taifa (kwa miaka 15), akiwa Katibu wa nchi za ukombozi wa
nchi za kusini mwa bara la Afirika.
Mwaka 1992 – 2000 –
amefanya kazi ubalozi wa Tanzania nchini Canada.
Mwaka 2006 -Naibu
Waziri wa Mambo ya ndani kwa muda wa miezi tisa.
Mwezi Oktoba – Disemba
2006 -Naibu Waziri wa Nishati na Madini.
Mwaka 2000 – hadi sasa
– Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa miaka 8 na nusu
Kimataifa
Mwaka 2007 – 2008
– Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mwaka 2008 –
Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri Nchi za Kusini mwa Afrika.
Mwaka 2008- 2009 –
Mwenyekiti wa Umoja wa Afirika (AU) wa Baraza la Mawaziri wa Afrika.
CHANZO NI MWANAHALISI OLINE
Hakuna maoni
Chapisha Maoni