Zinazobamba

HABARI KUBWA LEO,HALIMA MDEE AIBALALUA CCM BUNGENI,ASEMA MAZITO,SOMA HAPO KUJUA

Mbunge wa Kawe, Halima Mdee akitafakari jambo bungeni
Mbunge wa Kawe, Halima Mdee akitafakari jambo bungen

VIGOGO wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni miongoni mwa watu wanaojihusisha na uporaji ardhi ya wananchi na baadaye kusababisha migogoro. Anaandika Yusuph Katimba … (endelea).
        Kauli hiyo imetolewa leo bungeni na Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Halima Mdee wakati akiwasilisha maoni ya kambi hiyo.
         Akilieleza bunge hilo tathmini ya kazi za upinzani katika wizara hiyo kwa miaka mitano iliyopita (2010-2015) Mdee amesema, kila mwaka katika hotuba ya bajeti wamekuwa wakiliambia bunge na Watanzania kuwa, vigogo wa CCM wamekuwa ni sehemu ya uchochozi wa migogoro ya ardhi kutokana na kujihusisha katika uporaji.
          “Na kwa kuwa serikali hii ya CCM haina uthubutu wa kuchukua hatua, matukio mapya yanazidi kujitokeza na mwaka huu 2015/16 sakata la uporaji wa Ardhi linamhusisha Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, ndugu Leonidas Gama,” amesema Mdee na kuongeza;
        “Kiongozi huyu anaelezwa kuingia katika mkoa huo kwa mbwembwe nyingi akijipambanua kwamba anahitaji Halmashauri kutenga maeneo maalum ya uwekezaji!
         “Halmashauri zikiamini kwamba, kigogo huyu ana nia njema ya kuleta maendeleo zilipokea wito huo kwa mikono miwili! Moja kati ya Halmashauri hizo ni Halmashauri ya wilaya ya Rombo ambayo ilitwaa ardhi kutoka kwa wananchi na kuwalipa fidia ya jumla ya shilingi milioni 168.”
           Mdee amsema, kada huyo wa CCM alikwenda China (kwa gharama za serikali) ambapo alirudi na ‘wawekezaji’ wawili na kwamba, katika hali ya kushangaza juu ya ardhi iliyolipwa fidia kwa fedha za umma, ilianzishwa kampuni ya binafsi ya JUN YU INVESTMENT INTERNATIONAL COMPANY LTD.
Na kwamba, wanahisa katika kampuni husika ni Wang Zhigang – raia wa China waliokuwa na hisa 48,000), Feng Hu – raia wa China (hisa 49,000), na Muyanga Leonidas Gama – raia wa Tanzania (hisa 3,000). “Huyu Muyanga Leonidas Gama ni mtoto wa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,” amesema.
Mdee amesema, kwa taarifa za ki-inteligensia ambazo Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inazo; zinaonesha kwamba ‘wawekezaji hao wa kichina’ walilipa shilingi milioni 500 kama fidia kwa wananchi katika ardhi hiyo hiyo na kuwa, Halmashauri ya Rombo ililipa shilingi milioni 168 milioni na kudai, fedha hiyo mpaka sasa haijulikani ipo wapi.
“Mheshimiwa Spika, Kama hiyo haitoshi; Kigogo huyu pia anahusishwa na tuhuma za kutaka kufanya ufisadi katika eneo lililopo Kilacha (linalogusa jimbo la Vunjo na Rombo) lenye ukubwa wa hekta 2700. Eneo hili lilikuwa mali ya ushirika uliokuwa ukifahamika kwa jina la LOCOLOVA.
“Wananchi wanaishi na kufanya shughuli zao za kila siku!! Eneo hili linanyemelewa kwa udi na uvumba na kigogo huyu kwa kisingizio cha uwekezaji! Taarifa ambazo Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inazo ni kwamba; mbinu alizozitumia katika uporaji wa ardhi ya Wananchi wa Rombo ndizo anazotarajia kuzitumia tena katika eneo hili,” amesema.
Akizungumzia mafanikio ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwa kipindi cha maiaka mitano (2010-2015) amesmea, kambi hiyo itakumbukwa kwa kazi nzuri ya kutoa mawazo na fikra mbadala kwa ajili ya kuboresha utekelezaji wa majukumu yaliyopo chini ya wizara hiyo.
Hata hivyo, kutokana na ugumu wa Serikali hii ya CCM wa kukiri udhaifu, amesema imekuwa ikibeza ushauri mzuri wa kambi hiyo na hivyo kuacha mambo mengi kuendelea kuwa hovyo.
“Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni itakumbukwa kwa kuibua kasoro na matatizo mengi chini ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa lengo la kuitaka serikali ambayo kimsingi ndiyo yenye dhamana na yenye mamlaka ya kukusanya kodi za Watanzania itatue kasoro na matatizo hayo ili wananchi waweze kunufaika na rasilimali ardhi yao na kuishi kwenye nyumba zenye staha kwa mustakablali mwema wa maisha yao.”
Miongoni mwa mafanikio hayo ni pamoja na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kukemea na kulaani uporaji na ugawaji holela wa ardhi ya Watanzania kwa mataifa ya nje chini ya usimamizi wa serikali kwa hila au kisingizio cha uwekezaji.
Akifafanua matatizo ya ardhi sehemu mbalimbali Mdee amesema, Bara la Afrika ambalo ndio mlengwa mkuu wa mkakati huu wa uporaji wa ardhi linaongoza kwa kuwa na “mikataba” 754 inayojumuisha eneo lenye ukubwa wa hekta milioni 56.6 , ikifuatiwa na Bara la Asia lenye hekta 17.7 milioni, huku Bara la Amerika ya kusini likishika nafasi ya tatu kwa kujumuisha ardhi yenye ukubwa wa hekta milioni 7.
“Mheshimiwa Spika, Tanzania ni miongoni mwa nchi 11 ambazo zinaongoza kwa kupokea maombi mengi zaidi ya ‘wawekezaji’ . Nchi nyingine ni Sudan, Ethiopia, Msumbiji , Madagascar, Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Katika Bara la Asia nchi zinazoongoza ni Philippines, Indonesia na Laos,” amsema.
Hata hivyo amesema,  kwa mwenendo huo wa uporaji wa ardhi unaoendelea duniani na hapa nchini, kambi hiyo inaitaka serikali kuchukua tahadhari mapema kuilinda Ardhi ya Tanzani “isije ikachukuliwa na wageni na watanzania wakabaki kama watumwa ndani ya nchi yao.”

Chanzo ni mwanahalisi oline

Hakuna maoni