MWANDISHI SAED KUBENEA AMLILIA MAREHEMU KAMUKARA,ASEMA YAMOYONI,SOMA HAPO KUJUA
![]() |
| Marehemu Edson Kamukara enzi wa uhai wake akiwa kazini |
Gwaji la masuala ya
Habari nchini ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hali Halisi Publishers Limited
(HHPL), wachapishaji wa magazeti ya MwanaHALISI, MSETO, MwanaHALISI ONLINE na
mtandao wa MwanaHALISI Forum,Gazeti la Mawio Saed Kubenea ameshindwa kujizuia hisia na
kudosha kilio baada ya Kusikia Msiba wa Mfanyakazi mwenzake Edson Kamukara
Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo
Akitoa kilio hicho mbele ya changu
Mwandishi Kubenea huku akiongea kwa uchungu amesema
“Nimepokea kwa masikitiko makubwa
taarifa ya kuondokewa na mwenzetu Kamukara ambaye tulimfahamu na kumpenda.
Nilianza kufahamiana na Kamukara wakati
akiwa gazeti la Tanzania Daima. Namfahamu kama mchapakazi, mwadilifu na mkweli.
Alikuwa anashindana kwa hoja.
Yeye ndiye alikuwa mhariri wa kwanza
wa gazeti hili. Niliongea naye kwa simu mara ya mwisho Jumapili iliyopita,
wakati akiwa nyumbani kwao Bukoba, mimi nikiwa njiani naelekea Dodoma.
Ni katika mazungumzo yetu hayo,
ndipo aliponieleza kuwa alikuwa anasumbuliwa na malaria.
Ni mmoja wa waandishi wachache nchini
walioamini kwamba maadili ya uandishi hayatungwi na serikali wala wanasiasa
wenye uchoyo wa kuandikwa kwa mapambo, bali wanataaluma wenyewe.
Tulizungumza mengi kuhusu kazi,
lakini nikamtaka ajipumzishe zaidi na kuhakikisha kuwa anapata matibabu ya
kutosha.
Nilikuwa nampigia simu usiku wa
manane Kamukara kumweleza kuhusu habari ambayo tulipaswa kuijadili, kesho yake
alifika ofisini saa moja asubuhi.
Kwa kweli, alikuwa na bidii sana na
kazi. Alikuwa tegemeo kwa kampuni na pengo alilotuachia, ni vigumu kuliziba.”
Kubenea anasema, mpaka sasa,
haijajulikana wazi, sababu ya kifo cha mwandishi na mhariri wake, ingawa
anachofahamu ni kuwa alikuwa anasumbuliwa na malaria.
Anasema, Kamukara alirejea jijini
Dar es Salaam leo asubuhi kutokea Bukoba, ambako alikwenda kumjulia hali mama
yake mzazi ambaye ni mgonjwa.
Taarifa zinawanukuu majirani
wakisema, Kamukara alijisikia vibaya wakati anaenda dukani kununua dawa, ghafla
alianguka ambapo majirani walimsaidia kumpepea na baade kumpeleka kwake ambako
alipumzika hadi alipopata nguvu.
Hata hivyo, ghafla majirani walianza
kusikia kishindo ndani ya nyumba hiyo na baada ya kuingia ndani, walimkuta
akiwa ameanguka, huku fulana aliyokuwa amevaa ikiwa imeungua moto na yeye
kutoka damu nzito iliyotapakaa kwenye sakafu.
Aidha, televisheni ilikuwa
imepasuka, pamoja na vifaa vingine vidogo vidogo vya ndani navyo vilikutwa
vimepasuka, jambo ambalo
linaonyesha kama kulikuwa na purukushani au alikuwa akivunja vitu hivyo.
Edson Kamukara, amefariki dunia
jana Alhamisi, majira ya saa 12 jioni, nyumbani kwake, Mabibo jijini Dar es
Salaam.
Msiba wa marehemu Kamukara uko nyumbani
kwa dada yake Makongo Juu, jirani na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania
(KKKT).
Katika maisha yake ya
uandishi wa habari, Kamukara alifanya kazi katika vyombo vingi kikiwamo gazeti
la Majira, Jambo Leo na Tanzania Daima. Alijiunga na MwanaHALISI ONLINE,
Februari mwaka huu.
Tutaendelea kuwapa
habari zaidi

No comments
Post a Comment