HABARI KUBWA LEO-RAFU MBAYA YA PINDA,AFUJA KODI ZA WATANZANIA KWENYE URAIS WAKE,SOMA HAPO KUJUA
| |
ANAYEJIITA
na Kuitwa mtoto wa Mkulima,Waziri mkuu Mizengo Pinda imebainika anatumia Pesa
za walipa kodi katika harakati zake za kutaka Urais ndani ya Chama cha
Mapinduzi CCM,(Mtandao huu unafahamu),Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo
Waziri mkuu Pinda ambaye ni miongoni mwa
Makada wa CCM walitangaza nia ikiwemo kuchukua Fomu na kwa sasa yupo mikoani
mbali mbali akitafuta wadhamini 450 Katika Mikoa 15 ya Tanzania Bara na
Visiwani.
Kwa mujibu wa Mtoa taarifa wetu wa
Mtandao huu aliyoko kwenye Ziara ya Pinda kusaka Wadhamini ameupasha mtandao
huu kwamba Kiongozi huyo amekuwa akitumia mafuta ya Serikali,Mgari ya Serikali
pamoja na Watumishi wa Serikali.
“Yaani kinachofanyika huku ndugu yangu
ni kama kazi ya kusaka Wadhamini imekuwa ya Serikali hapa Kodi ya Serikali
inatumika,kughalamia mafuta,kuwalipa madereva hawa mpaka mtu unajiuliza hivi
anafanya hivi kwa misingi ipi wakati mambo ya chama haya husiani na
Serikali?”amehoji
Mbali na kutumia Mafuta yanayotokana na
Serikali pia Waziri mkuu Pinda anatuhumiwa pia kuongozana na Kitengo cha Habari
kilichopo Wizarani kwake.
“Tena
ameongozana na Waandishi wa Habari wa Serikali,ambao wote wanalipwa kutokana na
Kodi zetu mpaka unajiuliza hivi anachafanya akikubaliki kabisa hawa ni
watumishi wa Umma sahivi wangetakiwa wawe wanafanya kazi za kusaidia umma,sasa
anavyowatumia kuwatafuta wadhamini ni kosa la Jinai na kukiuka Katiba ya nchi”
Pinda,ambaye kwenye utawala wake
anatuhumiwa kufumbia macho Uporaji wa Mabilioni ya Shilingi kwenye Akaunt ya
Tegeta Escrow iliyokuwa Benki Kuu pamoja na kutuwashughulikia watendaji wa Mkoa
wa Dar es Salaam waliuza Shirika la Usafiri la UDA kifisadi, pia anatajwa
kutumia wakurugenzi mbali mbali wa Halmashauri kumsaidi kumtafutia wadhamini.
No comments
Post a Comment